huzuni kuu mkoani kigoma

Ms Judith

JF-Expert Member
Dec 24, 2010
2,563
919
Baba aua wanawe watatu, ajinyonga kwa katani Send to a friend
Sunday, 09 January 2011 20:59
0
digg

Anthony Kayanda, Kigoma.
MTU mmoja anayefahamika kwa jina la Filbert Kafonogo (35), amewaua watoto wake watatu kwa kuwakata mapanga, kisha mwenyewe kujinyonga kwa kamba ya katani.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana na kuthibitishwa na polisi mkoani Kigoma, zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea Januari 4 mwaka huu, katika Kijiji cha Makere kilichoko Kata ya Nyamidaho, wilayani Kasulu, Mkoa wa Kigoma.

Kwa mujibu wa habari hizo, mtu huyo alifanya mauaji hayo shambani kwake baada ya familia yake kumtuhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mmoja wa mabinti zake wa kuzaa.

Habari zilieleza kuwa siku ya tukio baba huyo aliwachukua watoto wake hao na kwenda nao shambani ambako aliwacharanga kwa mapanga kabla ya yeye kujinyonga.


Watoto waliouawa katika tukio hilo kuwa ni Obadia Filbert (13) aliyekuwa anasoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Makere, na dada zake mapacha, Salome na Siwema (9), wanaosoma darasa la tatu shuleni hapo.

Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nyamidaho, Ramadhani Shabani, amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa mauaji hayo yalipangwa kufanyika Desemba 26, mwaka jana, lakini baba mzazi huyo aliahirisha ili waweze kuona mwaka mpya.

Alisema siku hiyo marehemu Filbert aliichukua familia yake na kwenda nayo shambani ambako alipanga kuwaua, lakini aliamua kuwaacha ili washerehekee mwaka mpya 2011.

"Alipofika huko, aliwalaza chini na kutishia kuwaua kwa kuwakatakata mapanga, lakini baadaye aliamua kuwaacha kwa maelezo kwamba anasubiri washerehekee mwaka mpya wa 2011," alisema.

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaka kutajwa gazetini alisema: "Taarifa za kupangwa mauaji hayo Desemba 26 mwaka jana zilijulikana baada ya kutokea Januari 4."

"Mauaji ndio tumepata taarifa kwamba huyu Maheremu (Filbert) alitaka kuiua familia yake yote kipindi cha Krismasi, lakini, akawaacha washerehekee mwaka mpya,"alisema na kuongeza:

"Baada ya kuona hivyo, mkewe aliamua kwenda kijijini kwake Kitagata ili aepukane na kifo na alimwambia mama mzazi wa marehemu muwewe, tukio hilo,"alieleza mkazi mwingine wa kijiji hicho.

Habari hizo zilieleza kuwa Januari 4, mwaka huu, Filbert aliongozana na baba yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Kafonogo Maengo kwenda nyumbani kwa mkewe huyo kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgogoro wao.


"Juhudi za kumshawishi yule mke wa marehemu kurudi Makere zilishindikana kwa sababu alikataa na ndipo Filbert baada ya kufika hapa kijijini, alitoa taarifa kituo kidogo cha Polisi Makere kwamba mke wake amekataa kurudi," shuhuda mwingine alieleza na kuendelea

"Polisi wakampa barua ya kumwita mke wake huyo ili wazungumzie tatizo hilo mbele yao kituoni hapo,"

Shabani alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa limewasikitisha wakazi wengi wa eneo hilo.


‘Nimetoka likizo nyumbani Mwanza na kukuta hili tukio la mauaji, lakini bado sijapokea taarifa rasmi ingawa ni kweli kuna mauaji yametokea na maiti za watoto wawili na baba yao aliyejinyonga, tayari zimepatikana na kuzikwa jana (juzi)," alisema Ofisa Mtendaji huyo na kubainisha kuwa wananchi wanaendelea kutafuta maiti ya mtoto mmoja wa kiume ambayo haijapatikana.
Ofisa mtendaji huyo alisema maiti ya mtoto mmoja anayejulikana kwa jina la Salome ilikutwa katika kibanda cha marehemu na maiti ya mtoto mwingine aliyetajwa kwa jina la Siwema ilikutwa umbali mrefu kutoka katika nyumba yao iliyopo mashambani, sehemu iitwayo Nyarulilika.


Alisema mauaji hayo yaligunduliwa na baba wa marehemu, Kafonogo Maengo ambaye alifika nyumbani kwa marehemu kuwajulia hali na kukuta hali ya ukimya.

"Alipofungua mlango, na kuingia ndani, alikuta maiti ya mjukuu wake Salome ikiwa imekatwakatwa na kitu chenye ncha kali," alisema ofisa mtendaji.


Alisema kutokana na hali hiyo Kafonogo alipiga yowe kuiomba msaada wa majirani na baadaye kutoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi cha Makere.

Kwa mujibu wa ofisa mtendaj huyo, marehemu amekuwa akiahidi kuwaua watoto wake na mkewe kwa sababu ambazo bado hazijajulikana ingawa wengine wanadai kuwa amekuwa akitumia madawa ya kulevya.

Polisi mkoani Kigoma imethibitisha mauaji hayo na kueleza kuwa upelelezi wa tukio hilo bado unaendelea kubaini chanzo chake

source: Baba aua wanawe watatu, ajinyonga kwa katani
 
hata sijui kwa nin watoto baada ya kutishiwa mapanga hiyo 26/12 waliendelea kuishi na mtu kaam huyo nyumbani! jamani, God have mercy on your people
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…