Megawatt B
JF-Expert Member
- Aug 23, 2011
- 259
- 69
kwa kiswahili.....mkuu unashangaa kinondoni? Mbona ndio barabara nyingi za kitanzania zinavyojengwa?
Ndiyo maana dar ikinyesha mvua maji kila mahali, hakuna proper drainage system.
kwa hiyo usimlaumu huyu pekee, ndio mainjinia wetu walivyo.
Inasikitisha sana. Barabara inayotengenezwa kutoka Namanga hadi Kondo pale Tegeta haina hata vijimfereji.
Wameshindilia udongo vizuri, sawa, lakini kama hakuna mifereji ya kupitisha maji ni bure kabisa.
Mvua zikija udongo wote barabarani utaondoka. Utaaalamu gani huu?
Udongo??? Hii kali! Ninavyofahamu mie barabara hazijengwi kwa udongo.Wanatumiaga gravel material ya kiwango G3, 7, 15, or above!
Hivi hiyo gravel (au changarawe kwa kiswahili) siyo udongo mkuu? Mbona tukisoma kidogo tunajitoa ufahamu na kujiona kama tunajua saaaaaaana. Ndugu yangu huo ni udongo unaochimbwa ardhini na kwenda kusambazwa barabarani kwa grader na kisha kushindiliwa kwa roller. Huwezi kutuambia gravel materials siyo udongo!!! ukisema gravel materials ya kiwango sijui G3, 7, 15, or above ni kama vile materials fulani zimetengenezwa kiwandani???? Huo ni udongo tu ambao umekua selected kwa sababu ya properties zake kwamba unakua compacted tofauti na mchanga.
Imekuuma ee?
I cant argue!!! you are mature enough to understand yourself.