Huu wimbo unanikumbusha mbali sana

Msema yote

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2013
Posts
448
Reaction score
301
Wakuu tukiwa tunaendelea na wikiendi, mwenzenu usiku huu nimekumbuka mbali sana baada ya kusikia wimbo wa Chicco -Ineed some money,

Nimekumbuka miaka ya tisini na kitu huko Tarime - Mara, Tanzania Babu yangu (RIP) aliikuwa akiupenda sana wimbo huo, kwa hakika nyimbo zinakumbusha mbali, kuna wakati alikuwa akiimba.

Pia unanikumbusha hukohuko Tarime shule moja ilikuwa jirani na CMG karibu na mto wenye mti mkuubwa ukiwa unaenda hospitali ya bomani ilikuwa ni academy ya kizungu miaka hiyo ya tisini kulikuwa na mwalimu aliitwa LAWI (sielewi yuko wapi kwa sasa) alipenda kuwaimbia wanafunzi wimbo huu

kwa hakika sukrani za dhati zimwendee mgunduzi wa muziki kwani aligundua kitu kinachoweza fanya ukakumbuka vingi sana.

Vipi ninyi wakuu nyimbo zipi zinawakumbusha wapi na mnakumbuka nini?

NB. Yamkini wapo wataokumbuka majonzi, poleni sana kwa hilo lakini ni vizuri mkachangia ili tupate burudika sote kwa nyimbo za kila mmoja kwani wenda wimbo wako ambao ni huzuni ukawa kumbukumbu ya furaha kwa mwingine na kufanya siku hii ya leo kupitia uzi huu kuwa ya furaha kwako na kwetu sote kwani mwishao utaamini ya nyuma yalitokea ili leo itimie, yalitokea ili leo uwe ulipo, yalitokea ili upate faraja tumaini na nguvu ya kufika mbali zaidi. Lengo si kukumbushana machungu bali kuburudishana kwa kumbukumbu zilizosababisha tufike leo tulipo.

Tafadhali.
Majungu, kejeli si mahala pake tuchangie kistaarabu, kwa maana ni kiendi hivo yatupasa kupumzika, kujiliwaza na kufurahi kwa maana hiyo haitakuwa ustaarabu ukikosa ustaarabu

Karibuni .

 
Last edited by a moderator:
Ulikuwa unaenda kuangalia wapi, kwa Matutu?
 
New Edition-little Beat Of Love Unanikumbusha Familia Tulivokua Pamoja Tunaucheza
Michael Bolton-missing You Unanikumbusha Marehemu Mama Yangu
Spice Girls-viva Forever Nipo Darasa La Nne
Celine Dion-water From The Moon Huu Ndio Umenikumbusha Rafiki Angu Kipenzi Now Yupo Angola Kipindi Hicho Tulikua Wote Pale Kimandolu
 


pole sana kwa kumbukumbu ya mama, hongera pia kwa kuweza kumbuka rafiki yako alie angola kwa sasa, pia tungependa utafafanulie kuhusu familia mliokuwa mkicheza nani alikuwa mchezaji mzuri?
 
Kuna Kaka Etu Saiv Yupo TRA Moshi Alikua Anadance Mpaka Raha Japo Nilikua Mdogo Ila Nakumbuka Vizuri Mwingine Ni Dada Yangu Yupo Azania Bank Now Huyu Alikua Anaimba Wimbo Wote Wa Joyce Sims-come Into My Life msema_yote
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…