Wakuu hili jambo la ajabu sana kwa taasisi inayojinadi kwamba inatoa elimu fulani halafu inademonstrate kiwango kibovu kabisa kwenye taaluma hiyo hiyo.
Unakutana na front page ina WORD ART na contents hazionekani. Kama hukuwa makini kuona kuwa kuna scroll bars kulia na chini, basi unaweza kudhania hamna kitu. Kumbe kichefuchefu cha contents kimefichika. Yaani ni sawa na kuwa na presentation ya A3 kwenye screen ya A4.
Kwa institution kubwa namna ile, yenye vitengo lukuki halafu unakuwa na website shallow as if ni wanafunzi wa wiki ya kwanza wanajaribu jambo kwa kweli ni aibu. Just kick the link to see kichefuchefu cha chuo kinachofundisha Graphic Design, Web Designing, blah blah blah!
Hii nchi imeoza kila sehemu na sasa inanuka. Kazi za kupeana ndio shida yake hii, wote tunaonekana hatuna akili
Sasa mbona mambo madogo madogo tu yanatushinda hadi yanachefua. Yaani nia ya kufungua website yao ilikuwa nitafute taarifa ya kozi fulani hapo VETA, lkn nimeambulia kichefuchefu. Ya NIT ndio iko likizo kabisa, firewalls za PC yangu zimeiblock. Na wao pia wanafundisha IT.