Awiiiiii Uwiiiiiiiiii awoooooooooooo, ni vilio kila kona.
Vihana, wazee nao, aliye salama hakuna,
vilio maombolezo, mazikoni twapishana.
Tumwendee Mungu Baba, yeye ni mwenye rehema.
Awali katika tunakumbuka, virusi vilisheheni,
Pamoja tulianguka, tukaenga magotini,
Pasipo kuwa na shaka, pembezoni na mijini,
Mungu aliturehemu, dunia kuishangaza.
Imetupasa kujua, Mungu ni mwenye haki,
Huponya tukimwendea, ila uovu hataki,
Ataondoa balaa, na salama tutabaki,
Tukimrudia Baba, taif litaokoka.
Sisi sote tumekosa, tumefanya machukizo.
Uovu tumetakasa, hila tumefanya nguzo.
Kila kukicha ni visa, uharifu ni gumzo,
Kwa macho tunayaona, malipo ya wetu uovu.
Wanaume wanawake, kabila na rangi zote,
Mungu na tumkumbuke, hata ukiwa fungate,
Ashushe upanga wake, la sivyo twaisha sote.
Tukimwomba na kutubu, Mungu ataturehemu.