Klabu ya Singida Black Stars kupitia kwa Afisa Habari wake Husein Massanza imesema mshambuliaji hakuna timu Tanzania yenye uwezo wa kumnunua mshambuliaji wao Jonathan Sowah na kubainisha kuwa kama kuna timu inajiweza ije mezani na kitita cha Tsh bilioni 2.6.
"Ikitokea klabu inakuja inataka kumnunua (Jonathan Sowah), inaona inajiweza weza, dau mezani ni Dola za Kimarekani milioni 1 (Tsh. bilioni 2.6). Tunathubutu na kujiamini tukisema kwamba kwa Tanzania hakuna klabu yenye uwezo wa kutoa bilioni 2.6." Massanza
Hata hivyo, inaripotiwa kuwa Simba SC tayari wamemfuata mchezaji huyo na project nzuri, na kijana amekubali bila kusuasua. Vyanzo vimedokeza kuwa dili limekamilika, na sasa ni rasmi kwamba msimu ujao Sowah atavaa jezi ya Mnyama.