Kwanza naungana na Mh Kikwete kwa dhana ya kutatua "migogoro" kidiplomasia,
Lakini nimefedheheshwa sana na pendekezo la kumuomba Mseveni kuwa msuluhishi wa mgogoro huu,
Mgogoro wa Rwanda na Tanzania hauhitaji Tanzania tuombe suluhu,
Hii ni fedheha kwa taifa letu huru kwasababu kuu mbili,
1) Mseveni ni mbia wa mkataba wa Lemera wa kuigawa na kuiuza Kongo uliosainiwa vilima vya virunga Kaskazini Mashariki mwa Goma Lemera kati ya Paul Kagame, Yoweri Mseveni na Laurent Kabila, hivyo Mseveni anamaslahi kwa Kagame hawezi kuwa refa wa haki kwa hili,
2) Vita vya M23 na Jeshi la serikali ya Kongo ambako UN imepeleka majeshi yake huko (Tz na SA) Tanzania ikipeleka Bataliani 1 ya JWTZ ni kuwa Kagame na Mseveni wanahusika kwa asilimia 100,
Ripoti ya CIA,UN,HRW na nyaraka za kijasusi za Tanzania zimethibitisha pasina shaka kuwa Uganda na Rwanda zinawafadhiri waasi wa M23 ambao 90% ni Wanyarwanda kwa malengo ya kuiba raslimali za Kongo,
Mpaka hapo Mseveni ana maslahi na mgogoro wa Kongo ambao ndio chimbuko la mgogoro wa Tanzania na Rwanda, Hivyo hawezi kuwa refa wa haki kwa hili.
Ikumbukwe juzi 28/8/2013 tumempoteza mwanajeshi wetu (Meja) aliyeshambuliwa kwa kombora la M23,
29/8/2013 majeshi ya UN yamepamba uso kwa uso na majeshi ya Rwanda yaliyovuka mpaka kwenda Kongo kwa sababu ambazo Rwanda haijatoa ufafanuzi stahiki,
Inatia simanzi kuona serikali inapiga magoti na kusulubiwa bila kosa na Kagame,
Binafsi napinga Tz kuomba suluhu na zaidi napinga Mseven kuwa msuluhishi wa mgogoro huu,
Tanzania ibaki na msimamo wake kuwa haikumkosea Kagame,
Rais wangu acha ukigeugeu unatutesa watanzania tunaoamini na kusimamia imani ya nchi yetu takatifu tuliyopewa na Alha,
Kagame mambo yakizidi unga yeye ndie anatakiwa kuomba suluhu, na msuluhishi asiwe Mseveni!
Sisi ni Taifa huru na lenye nguvu Afrika Mashariki na Kati,
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika