Ticha mbona tangazo lako umeliweka kama ni kitu Haramu. Mbona unaandika kama hauko sereous mwalimu.
Jaribu kujiuza zaidi kupitia tangazo lako. Liandike in such a way umkomvisi mtu akuletee mtoto wake, usimpe mtu nafasi ya kudauti uwezo wako.
Katika tangazo lako ilitegemewa vitu vifuatavyo viwe clearly stated:
1. Location yako ikiwemo mkoa ulipo na uwezekano wa kumfuata mteja alipo
2. Wateja wako ni wanafunzi wa chekechea, msingi, sekondari au chuo.
3. Malipo yako ni kiasi gani na unalipwa kwa siku, wiki, mwezi au mwaka.
4. Jinsia yako
5. Experience yako ya ufundishaji na mafanikio uliyowahi kupatia watoto kwa kuwafundisha. Hata kama hujawahi kufundisha ndio unaanza basi say so na ukweli wako utakulipa
Siri ya well written tangazo ni kubwa Sana mdogo wangu. Hebu kaa Chini andika tangazo zuri. Kuna mtu hata kama hajawaza kumtafutia mtoto wake tuitions anaweza kabisa vutika sababu ya tangazo lako