Mojapo ya makundi hayo ya waasi, lijulikanalo kama South Sudan Liberation Army(kifupi -SSLA) likiongozwa na Peter Gadet linadai kuwa linapiga vita rushwa, ukosefu wa maendeleo na umiliki wa nyadhifa unaofanywa na kabila la Dinka.
Makabila ya Dinka ndiyo kabila moja kubwa kuliko yote ya Sudan ya kusini, na linalaumiwa kwa kushikilia nyadhifa nyingi muhimu katika jeshi la kusini pamoja na serikalini.
Kiwango kikubwa cha fedha hutumika kwa gharama za jeshi ikiwa ni robo ya mapato ya Sudan ya kusini, vilevile ni sawa na mara tatu ya jumla ya fedha zinazotumiwa kwa huduma ya Afya na Elimu kwa pamoja.
Kwa kifupi, hii ni sehemu tu ya wasiwasi unaoikabili serikali mpya wa makundi ya waasi pamoja na maadui wa kale katika utawala wa Sudan ya kaskazini huko Khartoum.
Ushauri lipunguzwe nusu
Ingawaje pesa nyingi hutumiwa kwa mishahara ambapo afisa mmoja wa Umoja wa Mataifa aliyeko Sudan ya kusini, David Gressley alinena hivi karibuni akishauri kuwa bora jeshi lipunguzwe kwa nusu baada ya Uhuru.
Mkono wa kaskazini upo?
Wapiganaji wa kundi la SSLA wamepambana na SPLA mara kadhaa karibu na makao yao makuu katika Jimbo la Unity.
Rais al Bashir
Kwa mujibu wa SPLA, makundi yote yanafanana kwa kitu kimoja;Yote yanadhaminiwa na aliyekuwa adui yao wote aliye mjini Khartoum.
Video iliyotoa sura ya hali ya mambo ilivyo huko Kusini mwa Sudan ilikabidhiwa kwa BBC na kiongozi wa waasi ambaye wakati huo alikuwa mjini Khartoum.
Ikiwa kuna ukweli au hata kama hapana ukweli, serikali ya Sudan ya kusini inaonelea kila hatua ya njama inayofanywa na wakuu wa Khartoum na yote haya yakiashiria uhusiano mbovu baina yao.
Katika kipindi cha vita vya miongo miwili, eneo la kaskazini lilikuwa na tabia ya kuyapa silaha makundi yanayohasimiana ili kulilegeza jeshi la SPLA.
Riek Machar
Hata Makamu wa Rais wa Sudan ya kusini, Riek Machar wakati mmoja alijitenga kutoka SPLA.
Hata hivyo Chama cha NCP cha Rais Omar al-Bashir kinakanusha kuwa kinaunga mkono kizazi kipya cha makundi ya waasi.
"Peter Gadet na wengine kama yeye hawakuwa sehemu ya Chama cha Rais Bashir cha NCP wala jeshi la Sudan, alikuwa ni sehemu ya mgambo wa SPLA, walioasi kufuatia kuibia kura baada ya Uchaguzi mkuu wa Sudan ya kusini, kwa mujibu wa afisa wa Chama cha NCP Ibrahim Ghandour.
Habari zisizokuwa za kufurahisha ni kwamba waasi hao wanapanga kutumia silaha zao kabla au baada ya sherehe za Uhuru wa Sudan ya kusini.