Karibu sana, subiri Mohammed Shossi na Miss Judith wakukaribishe kwa ushairi..Hodi Hodi jamvini,
Naomba Nipokeeni,
Pamweni Nijiungeni,
Nipate Kujifunzeni.
Mara nyingi nlitembelea,
Maoni nkajisomea,
Jukwaa nkajipendea,
Maamuzi nimefikia.
Majukwaa mefuatilia,
Yote yamenivutia,
Sinalo la kuchagua,
Yote ninayasifia
Nimepita mapenzini,
Mengi meyasomeni,
Sikuacha Siasani,
Hakika mefaidini.
Nimelikata shauri,
Jukwaa nimelikiri,
Nasema kwa kusitiri,
Jukwaani ntakariri
Hivyo napiga hodini,
Nikaribisheni jamani,
pamoja tujiungeni,
Taifa tulijengeni.
Bombu