Na vipi unapokuwa na namba ya simu ya mtu wakati yeye hajui kama unayo namba yake, siku unawasiliana naye kwa mara ya kwanza swali la kwanza ni; "nani kakupa namba yangu?". Silipendi kabisa hili swali.
Namba ya simu haiwezi kuwa siri wala ya binafsi. Kama unawasiliana na watu mbalimbali na wengine hata huwajui lakini wakitaka kukupigia au ukitaka kuwapigia unaweza. Sasa inakuwaje siri?
Nijuavyo mimi lengo la simu ni mawasiano,Inakuaje kwamba namba ya simu ionekane ni kitu cha siri sana kiasi kwamba watu wengi hukataa kuweka wazi au kupewa mtu mwengine bila ridhaa yake?
Kwani tatizo ni nini?
Kwa mimi namba yangu sio siri wala binafsi ila ukipiga simu haipokelewi kabisa we jaribu ujutee ukituma text wajibiwa za kumwagaaa tu.
Kwa wasumbufu huwa nawashughulikia kwa majibu ya pasua kichwa mpaka wachoke wala huhitaji kuiomba ipo huru kwa yeyote kwa mawasiliano yoyote wewe anza tu text zako upendavyo wala huuliziwi ulipoipata au aliyekupa utaulizwa wewe tu jina au jinsia yako inatosha na hili haliulizwi siku ya.mwanzo baada ya kuchat kwa muda kidogo.
Ukiona mtu anaifanya namba yake siri ujue huyo hana ujanja wa wasiwasi wake tu. Na pia hachererwi kuibadilisha kwa wasiwasi huo huo
Jinsi ilivyo namba za simu ulizo nazo asilimia 98 ni wale watu unaoendana nao ktk hali yako kimaisha.
Mifano:
1.anaetumia jiko la umeme hawezi kua na namba ya muuza mkaa.
2.Mvuvi hawezi kua na namba ya mchimba madini.
Labda wawe wana undugu.