Historia ya X-ray

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
X-radiation (imetengenezwa na X-rays) na inatokana na electromagnetic radiation. X-rays mara nyingi zina wavelength kati ya 0.01 na 10 nanometers, ikiwasiliana na frequencies kati ya 30 petahertz mpaka 30 exahertz (3x1016Hz mpaka 3x1019 Hz) na nguvu kati ya 100 eV mpaka 100 keV. wavelengths za X-ray ni fupi kulinganisha na za UV rays na ni ndefu kuliko zile za gamma rays. Katika lugha nyingi, X-radiation inamaanisha Rontgen radiatio, baada ya Wilhelm Rontgen, ambae sikuzote anapewa sifa kama mvumbuzi wa kifaa hicho, yeye alikipa jina la X-radiation ikimaanisha radiation ambayo haitambuliki. Maandishi ya X-ray kama ijulikanavyo kwa lugha ya Kiingereza yanaweza kuandikwa kama x-ray, X ray au X-radiation.






Wilhelm Rontgen.

Wilhelm aligundua X-rays zikitokea kwenye Crookes tubes,(Crookes tubes zilitengenezwa na mwana physics wa Kiingereza aliyeitwa William Crookes), akifanya utafiti wa tube za kutoa mwanga mwaka 1875, wanasayansi walifanya utafiti wa cathode rays, hii ni nguvu ya umeme unaowaka na kuzima na ilipekea kutengenezwa kwa tubes. Crookes tube zilitengeneza umeme kwa kufanya ionization ya hewa kwenye tube zenye nguvu kubwa ya DC voltage kuanzia kilovolts na 100kV. Voltage hii ilitoka kwa kasi na kufanya electrons kuja kutoka kwenye cathode na zilikuwa na nguvu sana kiasi cha kutengeneza velocity ya kutoksha kutengeza X-rays zilipoachwa kwenye anode au ukuta wa kioo. Crookes tubes za mwanzo zilizalisha X-rays radiate, wanasayansi wa mwanzo waliweza kuona hayo na Wilhelm Rontgen alikuwa wa kwanza kuanza kufanya utafit wa kina katika hili mwaka 1895.

Kugundulika kwa X-ray kulihamasisha uchunguzi wa kina. Mwandishi wa maisha ya Rontgen Otto Glasser anakadiria kuwa mnamo mwaka 1896 pekeyake, kwa uchache insha 49 na articles 1044 zilizohusisha miale mipya zilichapishwa. Hii ni takwimu chache kama kila mtu atafikiria kuwa karibu kila gazeti duniani liliandika kuhusu uvumbuzi huu, jarida kama Science dedicating lilikuwa na articles 23 kuhusu hili kwa mwaka huo mmoja tu.

Wote wawili William Crookes (miaka ya 1880) na mwana physikia wa Kijerumani Johann Hittorf, kwa pamoja waligundua kuwa, tube za Crookes zikiwekewa photographic plates karibu ziliweza kuleta kivuli halisi, ingawa hakijawekwa kwenye mwanga. Hakuna kati yao aliyetafuta sababu au kuchunguza madhara yake.
 

Shukran Kwa kutupa mwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…