matumizi bila akiba, fedha hazitatui ukiumia
usupastaa ni mzigo wa mwiba, ukiubeba utaumia
hii dunia ina mambo, kama wasemavyo watu pori
ndo mana nikipata mpira basi kinachofuata goli
ujanja ukiuzidisha, si muda mfupi utaitwa mshamba
nilianza rap enzi hizo Sinza watu wanauziwa viwanja
unga ukamfunga kamba, mc hukatikia
pembamba
mwenzetu yule anaigiza, anauliza huu
wapi mwanga
sasa kwa ubishi na hasira kama Squizer mimi naja
kwa mshindo wa haja kama mvunjiko wa bawaba
nikienda chimbo haipiti wiki,yaani haizidi siku saba
huyu jamaa anaitwa muda, siyo raafiki wa mwanadamu
atakukosesha mavumba kama hauko on time
aaminiae kwa mdomo, siku zote haishi kutema
asante mola kwa hi sauti ya busara leo nasema
maisha kama kioo, ukiyachekea nayo yanacheka
na hii mipaka bila uhuru Afrika ni utumwa wa kifikra
chagua ufe Kijerumani anguke na tai shingoni
au Mchaga anayeshinda njaa wakati anazo hela mfukoni
huu sio wakati wa kujaribu, wenzako wanafanya kweli
au hujui bahari tulivu haimpimi nahodha wa meli
ona wasio na hatia wanapelekwa gerezani
halafu wavunjaji wa sheria wanaachwa wa jazane uraiani
we unadhani, nuru bandia za shetani zitaharibu imani
za wale wanaougua na kulia juu ya makosa ya mtu fulani
maneno yangu mi ni ya moto, na mdomo wangu hauna friji
yananitoka bila yakupooza, najiuliza nimeyameza vip
By fid q