Hili ni sawa katika elimu?

The Mig

Senior Member
Joined
Jan 7, 2017
Posts
131
Reaction score
217
Wana bodi naomba kwa mara hii tu ya kwanza niseme kitu,
nisikae kimya bure huku nisema pembeni kama majungu,
kwa haya niyaonayo katika elimu na sera zake za sasa.

Nataka kujua kama elimu yetu inapanda au inashuka
hasa kwa kipindi hiki toka dada Nalichako apewe wizara hii.

Pia nataka kufahamu vigezo vinavyotumika kutambua kupanda au
kushuka kwa elimu ya jamii au nchi mahalia.

Hapo awali kabla yake niliona sera ya elimu iliyojikita
zaidi kuhakikisha hata yule mwenye uwezo mdogo wa kukariri
what is archimedes principle anapata nafasi ya kusonga mbele.

Mazingira ya ku re sit mitihani ilikuwa rahisi sana
kama unatafuta credit moja, basi unakomaa na hiyo hiyo
na si kubeba masomo yote saba.
Mi hapa sipaelewi kabisa wadau.

Nadhani wazazi wanaopenda watoto wao wafanikiwe katika elimu
watasomesha sana hadi wafirisike.
Pili baadhi ya wanafunzi (walio wengi hasa wanaomaliza kidato cha nne) itawapasa kuzeekea madarasani.

Hivi kweli kupandisha elimu kunahitaji kubana na kuweka masharti magumu kwa wale wanaokosa fursa za moja kwa moja za kuendelea na elimu?

Hivi waliofanikiwa katika elimu mfano Nigeria wana masharti kama hayo?
Hivi nchi hii inataka kweli watu wake wawe na elimu inayowawezesha kutambua mazingira yao (ile ya chuo kikuu)?

Hofu ni nini ya kuweka mazingira magumu namna hii ya watoto wetu kujiendeleza? Ukizingatia mitaala iliyopo hairuhusu au kumwezesha aliyefaulu kutumia kile alichojifunza kujiajiri? Shida ni nini wadau? ni kupandisha viwango vya elimu kweli au kuna agenda ya pembeni ya kutengeneza wasomi wachache wa kuja kuwatumikia watawala?

Je hofu ni kutengeneza bomu la ajira kama mmoja wetu alivyowahi kuonya? kwa kuwa na wasomi wengi wasiokuwa na ajira kwa kuwa elimu yetu haimpeleki msomi kujiajiri hata kama akipewa mtaji, vinginevyo awe na kipaji binafsi.

Hapa siongelei VETA wadau, nazungumzia elimu yetu ya kumeza
ambayo inawafaa sana WAHADHIRI.

dada waachie watoto wetu wote wenye bidii wasome, ndiyo faraja yetu
hata kama watarudi kuungana na sisi kuvua dagaa na digrii zao, sisi tunajiVunia hilo.

Natamani kulisongesha sana kwa yaliyo moyoni
ila hili naona kama taifa tunateleza mahali


Haya ni yangu mwenyewe The Mig
 
wadau wa elimu wanailalamikia sana sera ya elimu wanasema ni mbovu achilia mbali mazingira ya kupatia elimu hasa kwa shule za serikali
 
Elimu ni mbovu sana naomba wapandishe grade
 
 
mkuu ulimaliza mwaka gani na ulipata ngapi ???co unasema tu grade ziongezwe kwa lengo lipi??????

Mkuu bora umehoji
Nadhani hapa siyo kupandisha grade vipi. swali la msingi ubora wa elimu unapimwaje? na wenzetu wanafikiaje kuwa na elimu bora? pia kuongeza masharti magumu ya kutafuta credit ulizokosa ndiyo kuboresha elimu au kuipandisha?
 
wadau wa elimu wanailalamikia sana sera ya elimu wanasema ni mbovu achilia mbali mazingira ya kupatia elimu hasa kwa shule za serikali

Ni kweli hali hii ya elimu inanipa mashaka ya hatima ya wale wenye division 3
wakapata credit 2 za combination zilizokataa anataka credit 1 ili aweze kuendelea na kidato cha tano.
Unamlazimisha arudie masomo si chini ya 7 kutafuta credit 1. Hapo unakuwa unapandisha elimu kweli?
Mi kwa kweli sielewi lengo hasa la hii sera. Ni kero na yenye kubinya sana watu wakwame wasisonge mbele zaidi kutafuta vyeti.
 
Ndio maana watu wengine wanadharau wasomi wa Tz
 
Huyu dada Ndalichako hebu aangalie upya hili sharti lake la kutaka mtu arudie masomo
yote saba (7) ili hali anatafuta credit moja tu ili kombi yake ikubali.
Kama siyo sharti lake yeye mwenyewe achukue hatua ya kuhakikisha utaratibu
uliokuwa unatumika kabla yake unarejeshwa.
Kama ni sharti lilotokana na utashi wake au muono wake bianafsi basi aangalie upya
namna ya kuwafanya watanzania watoto wetu wapate credit walizo zikosa
si kwa kuwabebesha zigo kubwa tena wakiwa katika mazingira duni ya kujisomea (nyumbani)
 
Haya Mambo Yanaitaji wataalam Wa Elim Kuweza Kuyachambua kwa Uyakinifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…