Hiki kisa kimekaaaje wakuu???

torvic

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2016
Posts
4,484
Reaction score
11,174
Wakuuuu!
Hebu check hiki kisa cha kweli kabisa, alafu utaniambia imeka vp
Rafiki yangu mmoja alifanikiwa kuoa akiwa bado kijana kabisa, miaka 22-25 hivi
Na kwenye maisha yake ya ndoa kwa kweli alikuwa ana struggle sana kutokana ugumu wa maisha

Baada ya miaka kadhaa ndani ya ndoa mjamaa alifanikiwa kupata watoto mapacha, na kusema ukweli vile vtoto vilikuwa vizuri kweli

Lakini kutoka na maisha kuwa magumu na maisha yalizidi kuwa magumu baada ya kuja kwa vitoto hivyo viwili ilipelekea watoto kumwa mara kwa mara,
Kwa bahati mbaya sana mtoto mmoja alifariki kwasababu ya magojwa ya hapa na pale, kama wazazi wote waliguswa na msiba wa mwanao,

Kama mnavyojua misiba ratiba na utaratibu ukafwata kama inavyokuwa, wakazika na maisha yakaendelea

Sasa ilipita kama wiki hivi baada ya msiba nikakutana na rafiki yangu uyo aliyefiwa na mwanae wa miezi 3

Tukasalimia, baada yapo nikamwambia pole na msiba rafiki yangu... doooooh! (wandugu majibu yake aliyonipa ndio sababu ya mimi kuja hapa)
alinijibu akisema, Asante rafiki yangu lakini namshukuru mungu sana kwa kunipunguzia majukumu maana nilisongwa sana na maisha na watoto walivyokuja mapacha ndio nilizidiwa kabisaa! kwaiyo namshuru mungu kwa hilililo tokea...

na aliongea hayo maneno kwa kujiamini kabisa kana kwamba hakuwa na msiba hapo nyuma. nilichoka na niishiwa na pozi.

Hivi kweli wakuu maisha yanaweza yakakushika kiasi hiko mapak msiba wa mtoto wako ukamshuru mungu kakupunguzia majukumu??

au ndio matokeo ya kuoa ukiwa na umri mdogo ukipata matatizo unataka kudata??

Jamani hii imekaaje??
 
Kama sio story za kwenye kahawa ebu sema kisa kimetokea mwaka gani?
 
Kama sio story za kwenye kahawa ebu sema kisa kimetokea mwaka gani?
Boloyoung, kwanza mimi kahawa aipandi kabisaaa!
iko kisa ni cha ukweli kwa asilimia 800
 
Akili ikiwa bado ya kitoto huwa kila kitu unakiona sawa na huyu ndugu yako anaweza akawa ni utoto haujaisha kichwani kwake
 
Kwani umri sahihi wa kuoa ni kuanzia miaka mingapi mpaka mingapi?
 
Kama aliongea hayo huyo atakua ameathiriwa na kifo cha mtoto, amekua chizi.

Unaoa huku hauna mipango madhubuti ya kulea familia unatarajia nini?
Siwezi kumtukana kwakua naamini ni ukichaa unampanda.

Wenzake maisha magumu tumechukua uanachama CHAPUTA yakikaa sawa tutaukana uanachama na kuingia ndoani.
 
Kwani umri sahihi wa kuoa ni kuanzia miaka mingapi mpaka mingapi?
umri mzuri ni miaka 30-35, pia unashauriwa kuoa pale ambapo upo tayari kuoa yaani unaweza kulea mke na watoto.
 
same to me,
sababu kama hizi ndo zinanifanya nsiwaze hata kidogo ndoa.
 
Hapo ntakupinga kidogo, umeangalia zaid negativity ambazo ni chache lakn ukienda upande wa pili ( positivity), utasema bora kuoa na ukishaoa upate mtoto hapo utaona utamu wa kuoa. But kila mtu yupo sahihi kulingana na mtazamo wake broo. Huyo rafikiyo alikujibu vile koz akili yake ilikuwa bdo haijatulia baada ya kutoka matatizoni, ila baada ya mwaka kupita ukimkumbusha, utamgusa pabaya na atakuambia aliwapenda sana wanae.
 
hahah Castr, nikweli uliyoyasema lakini ukiingia CHAPUTA kutoka mpaka kwa msaada wa winchi ujue!
 
Hii imechuchumaa haijakaa.
 
Boloyoung, kwanza mimi kahawa aipandi kabisaaa!
iko kisa ni cha ukweli kwa asilimia 800
Dah....hv hizi avatar huwa mnaxitoa wp? nimecheka hadi nimesahau mada inasemaje!
 
na mtu mwingine angefikiria kama wewe ama kwa hakika usingekuwepo wewe leo hii. Tumsifu Yesu kristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…