Hii hata Lissu Mwenyewe haiwezi, maana amejaa chuki za wazi kabisa na si kwamba eti ana mpango wa kufanya kitu tofauti sana. Maana nimeshangaa vitu anavyoviongelea kwa uchungu kama kero, hajui kuwa imekuwa historia kwa sasa.
CCM inapigiwa kampeni kwa nguvu kubwa sana ya uongo LAKINI CHADEMA inajinadi yenyewe kwa hoja na sera.
CCM inatengenezewa mteremko wa wagombea kupita bila kupingwa LAKINI CHADEMA wanapambana kiume, hakuna aliyepita bila kupingwa.
CCM Inatumia rasilimali za umma katika kufanya kampeni zake LAKINI CHADEMA wanajibeba kwa mali na rasilimali zao halali za chama.
CCM wanalazimisha watu na kuwabeba kwenda kusikiliza hotuba za mgombea wao LAKINI kwenye mikutano ya CHADEMA watu wanatiririka wenyewe, wafanyakazi wanatoroka maofisini, wenye maduka na biashara wanafunga biashara zao na kujumuika kumsikiliza mgombea wa CHADEMA.
CCM katika kampeni hizi, ni chama pekee kilicho na hofu kuu LAKINI CHADEMA hakina hofu, No blaa blaa ni mwendo wa sera na hoja madhubuti.
ILANI ya CCM imerefushwa kwa kuongezewa na nyimbo 500 za kina Diamond platnamz, LAKINI ILANI ya CHADEMA imesheni hoja na vipaumbele vinavyogusa "Uhuru Haki na Maendeleo Endelevu ya Watu". Just to mention a little!