Hii ilinitokea mwaka 2002

Mgeni wa Mungu

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2015
Posts
1,233
Reaction score
1,296

Binadamu tuna majaribio mengi duniani, wakati nimeshamaliza kusoma mwaka 2000 kisiwani Pemba nilipata ajira ya kusimamia Guest house nikawa kama manager kipindi icho wageni walikua wengi na wengi walikua wazungu. Ilikua sa1 jioni niliwapokea wageni 2 wazungu walikua ni wale waliomiliki boti iliyokua inaitwa Sepideh. Hawa wageni niliwapokea nikawapa room nikaendelea na kazi zangu. Kwa mshangao mkubwa niliingia chumbani kwao nikakuta begi ya pesa iliokua wazi na dola zilizokua zimejaa mpaka juu kama picha inavoonekana. Kwa kweli nilishangaa sikuweza kuamini kama ni pesa za kweli au ni mtego. Wakati huo chumbani walikua hawamo wako chumba cha pili wanakunywa pombe. Nilijaribu kuzichezea noti za vibulungutu vya 100 vilivokua vimejaa. Kilichofata nikatoka ndani na kufunga mlango kazi iliyobaki nikawa nimeamua kuzilinda mpaka wamalize warudi chumbani kwao. Majaribu ni meng niliwaza sana lakini sikupata jibu sijui kama ni wewe ungefanyaje?
 
Uaminifu ni jambo la msingi sana nani ufunguo wa baraka nyingi...

Ulifanya vema kuzilinda mpaka waliporudi, vinginevo hata ungedokoa noti moja wala usingekua na amani na huenda usingefanya chochote cha maendeleo....

Maendeleo na maisha mazuri ni ndoto na tamanio la wengi wetu, lakini maendeleo hayo yakiwa yametokana na njia nyofu amani inakuwepo na furaha ya kweli inapatikana....

Ni vema kulinda uaminifu kwa gharama yoyote ile....
 
shithole countries..... huu msemo unanisikitisha, unaifikirisha sana mda mwingine. jioni njema mkuu
 
hii stori ukija kuwahadithia wajukuu wako wakati utakapo kuwa MZee ..haki yanani tena tarajia kunyeshewa na mvua ya matusi ..

tena jinsi hcho kizazi kijacho kitakavyokuwa ktk dimbwi la mmong'onyoko mkubwa wa maadili ..basii we jiandae tu kutukanwa mpaka na kuku ..
 
Reactions: rbt

Nilifanya kuweka ulinzi wa muda kwa sababu sikuwa peke yangu na tulikua vijana watupu. Nashukuru kwa kunichangia maneno ya msingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…