Jana tar.14.09.11 Serikali ya Ufaransa kupitia balozi wake hapa nchini imeisamehe serikali yetu deni la bilioni 21.8 na kuiomba Serikali yangu ilielekeze fungu hilo kwenye Elimu, Balozi huyo aliongea kwa Lugha ya kiswahili ambayo idadi kubwa ya wananchi wetu wanauelewa nayo. Chanzo cha ITV habari 2:12 usiku. Swali langu Kwa serikali, Je kauli za kuishiwa fedha zitakoma?