Heshimu fedha ya Tanzania

MKALI WA MAMBO

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
211
Reaction score
146
Nimeaoma Taarifa kuhusu kukamatwa kwa Mtangazaji Soudy Brown na Maua Samma na vyombo Vya dola kwa kosa la "KUHARIBU MALI" mara baada ya kuonekana kwenye Video Wakilusha Hela na kuzikanyaga:

Well, kama ilivyo kwa serikali zote za mataifa mengine Duniani Serikali ya Tanzania pia huingia Gharama kutengeneza Fedha aidha za not au za Coins, na hata zinapochoka au kuchanika inabidi iingie Gharama kuchapisha zingine, na Gharama hizo ni kodi za wananchi, je tuache watu waharibu kwa kukusudia ?

Kifupi hela ya Tanzania iliyopo Mfukoni Mwako ni Mali ya serikali chimi ya BOT...Unachomiliki wewe ni thamani (value) ya hiyo fedha tu...Zingekuwa ni Fedha za Marekani USD au YEN za japan kungekuwa hamna kesi kwa hapa kwetu.

Kisheria Mtu ana Uhuru wa "Kutumia Fedha zake vile atakavyo lakini hakuna Uhuru wa kuzichakaza au kuziharibu fedha hizo kwa Makusudi hata kama Zipo Mfukoni Mwake.

Ni wakati sasa Benki kuu itoe Elimu kwa Umma juu ya Mambo yahusuyo Fedha ya Tanzania.
 
Sudi kapata tabu. Anyway Kuna picha ya bashite nimeiona ana bastolA sijui ni ya kweli
 
Mkuu hivyo vyote vipo katika kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwA marekebisho 2002. NA tukumbuke kutokuijuasheria haiwezi kukufanya kusamehewa kosa
 
Kick....waliziiba kwenye viroba mbona hatujui zilipo. Kama wamezichoma au wanatumia majumbani mwao kama toilet paper tutajuaje? Hilo jeshi la kuomba poo kwenye uchunguzi..
 
Kuna mtu asiyeheshimu pesa usawa huu????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…