Nasir Jones (amezaliwa tar.
14 Septemba 1973) ni mwanamuziki wa rap na mwigizaji kutoka nchini
Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake kisanii kama
Nas. Zamani alikuwa akijiita
Nasty Nas. Nas ni mtoto wa mwanamuziki wa jazz wa zamani Mzee
Olu Dara. Alizaliwa na kukulia katika nyumba za miradi za mjini (nyumba za watu wenye kipato cha chini)
Queensbridge, New York.
Nas alisaini mkataba na studio ya
Columbia Records mnamo mwaka wa
1994, na kutoa albamu yake ya kwanza ya
Illmatic. Albamu ya Illmatic ilipata kuwa bora na kufahamika zaidi na mauzo bora.
Baadaye albamu kadhaa za Nas zilifuata. Albamu hizo ni pamoja na
It Was Written ya 1996,
I Am... and Nastradamus ya 1999, na
Stillmatic ya 2001. Nas alikuwa mmoja kati ya wanakundi la muziki wa rap na hip hop -
The Firm, ambalo limejumlisha wasanii wengine kama vile
AZ,
Foxy Brown, na
Nature. Ingawa, kundi halikufanya kazi nyingi na badal yake wakatoa albamu moja tu ya pamoja.
Kuanzia mwaka 2001 hadi`2005, Nas alihusishwa katika ugomvi mkubwa na rapa mwenziwe Bw.
Jay-Z. Marapa wote walikuwa wakishambuliana kwa kutumia nyimbo zao.
Wawili hao ugomvi wao ukaja kwisha baada ya kualikwa katika tamsha la muziki la New York City-area hip-hop za vituo vya redio. Nas akasaini mkataba na studio ya Jay-Z maarufu kama
Def Jam mnami mwaka
2006.
Albamu yake ya kwanza akiwa kama mmoja wa Def Jam, ilitoka mwaka wa 2006, ikiwa na jina la Hip Hop is Dead, ikiwa imeambatana na albamu nyingine ya mwaka wa 2008, iliyokwenda kwa jina la
Untitled.
Albamu alizowahi kutoa.
Source: Wikipedia