katibu wa baraza la madiwani ni Murugenzi wa Halmashauri, kwa kifupi nafasi za afisa tarafa zinalazimishwa kuwepo tu ili kulinda cheo cha DC. hawa wanaripoti kwa katibu tawala wa wilaya hivyo kukamilisha team ya watu waliokuwa chini ya DC. Kwa kifupi hawana kazi za moja kwa moja za kuwahudumia wananchi kama ilivyo watendaji wa kata na vijiji. Kama huna option ya kazi nyingine nenda tu ukafanye hii kazi ila kwa maendeleo ya kitaaluma sikushauri ukawe afisa tarafa