Hebu waangalieni MAGAMBA....AIBU!!!

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
77,343
Reaction score
111,606


Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akikimbizwa na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma

Kwa ufupi

Vurugu hizo zilizotulizwa na Polisi wa Kutuliza Ghasia (FFU), zilitokea jana mchana katika uwanja huo uliopo karibu na Baa ya Mwanga, baada ya CCM kung'oa bendera ya Chadema iliyokuwepo uwanjani hapo, ili waweke bendera zao kwa ajili ya mkutano ambao ulikuwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM.


Source: Gazeti la Mwananchi
 


Kada wa Chadema Mkoani Dodoma, Arnold Swai akikimbizwa na wafuasi wa CCM jana, baada ya kutokea vurugu katika eneo la Mwanga baa, Dodoma

Kwa kweli hii haikubaliki.Angalia huyo jamaa alivyobeba hilo jiwe, utafikiri anakwenda kuua mbwa au mwizi.Siasa zetu zinakoelekea sio kuzuri.Hivi huyu jamaa aliyeumizwa akiamua kujipanga kwa revenge si itakua hatari.Inabidi watu waelimishwe maana ya siasa ya upinzani.
 
Inasemekana wafuasi wawili wa CDM waliumizwa kiasi cha kushonwa nyuzi...

 
ha ha ha ha halafu jamaa bado anawapiga chenga tu hapo. hakuna kurudi nyuma mpaka kieleweke
 
CCM wamejichukulia sheria mkononi . Hapo sheria vipi? na wanaonekana kabisa. Tundu Lisu upo?
 
Dah kuna lijamaa naona limenyanyua bonge la jiwe...sijui linanenda kubonda nyoka????
 
Wanatekeleza Sera ya Amani na Utulivu, Utawala wa kuheshimu Sheria (tena ukiiangalia karibu yote ni mijitu mizimaa!)
 
Jamani jamni huyoo alie beba jiwe sio Le MUTUZ Malecela kweli?naona wamefanana kwlei.Duh kweli ukwa mwanachama wa CDM yakupasa ujifunze ma karate na ma judo kwa saana ili uweze kukabiliana na hawa wafuasi wa chama cha WAFUUCCM.
 
CCM wote wana akili za kushikiwa. sasa utafikiria huyo jamaa mwenye bahasha anavyorusha jiwe, huyo mwenye bakashia inaonekana ameshalirusha, halafu yule jamaa wa mwisho kulia anakuja na bonge la tofari. So tuseme nia yao ilikuwa ni kuua? Walikosa polisi wa kuwatumia kama walivyozoea? Walikosa mapanga na chelisaw za kuchinjia kama walivyofanya Arumeru mashariki. Halafu ona hapa chini jinsi Rage alivyomkuda jamaa hii ni aibu kubwa kwa mbunge kufanya hivi. CHADEMA tuamuke, upole wetu utatumaliza. Bora tuzipige tu.

 
Mhhh, hawa ni lazima washitaki. Hao watu walioumizwa ni lazima wawashitake na Rage aliyetoa amri lazima apande kizimbani tena maana jamaa anaonekana haelewi Somo.

 
CHADEMA NI WATU WA KUPENDA VURUGU TUU by NAPE NNAUYE.wasioruhusiwa kuchukua sheria mkononi ni wapinzani tuu.
 









Hao kwenye Nyekundu utafikiri walikuwa wanapiga mwizi!kweli huruma kwao sifuri!
 

Attachments

  • KandawaChademaakikimbizwa 2.jpg
    53.1 KB · Views: 52
Halafu utasikia uchunguzi wa polisi umefanyika lakini hakuna ushahidi kama CCM ilifanya fujo au kujeruhi
 
Zamani mavazi ya chama yalikuwa yanavaliwa na watu wenye staha! ona sasa tunavyouza amani yetu kwa bei nafuu! Bendera inapokuwa na thamani kuliko uhai wa Mtanzania mwenzako. Sitarajii kama juhudi hizo za kutaka kutuongoza zinafaida na ustawi wetu, sanasana faida zenu binafsi ndio maana mko tayari hata kuuana. Mawe ya nini? shindaneni kwa hoja nasi tutawaunga mkono kutokana na uzito wa hoja wa kila mmoja wenu. Cheo ni dhamana mmekabidhiwa na mwenyezi mungu! mtatakiwa kutoa hesabu yake siku ya kiama. Ole wenu mnaochochea vita na machafuko ni heri kama msingezaliwa!
View attachment 81959

View attachment 81960


View attachment 81961

View attachment 81963

Hao kwenye Nyekundu utafikiri walikuwa wanapiga mwizi!kweli huruma kwao sifuri!
 
Mzee mwenye KIBANDIKO alianzaia huku...angalia anavyojipenyeza kutafuta nafasi ya kuleta vurugu zaidi

View attachment 81961

Akaendelea hapa kwa kurusha jiwe...hivi huyu mdingi sijui kama ana watoto, hata huruma hana

View attachment 81963
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…