Maiti aliyefukiwa asipoguswa na nzi hatatoa funza nijuzeni
Mkuu hii sayansi naikumbuka kwa mbali.... labda tu kuwa pamoja... ina maana wale funza wa chooni kama vyoo vya shuleni baadae (saint Kanumba) wanageuka kuwa nzi wakifika stage ya 4?
Mkuu kuna species mbalimbali za flies wanaoishi na kutaga mayai mazingira tofauti tofauti,funza wa vyooni hutokana na aina mbili za flies ambao ni housefly(Musa domestica) na Blowfly,hawa upenda kutaga mayai sehemu zenye uozo(wa mimea na wanyama)na kwenye vinyesi,mayai yatabadilika kuwa maggots(larva stage) ambao ndio funza na kama watapata nutrients wakikamilisha stage zilizobaki uwa inzi ingawa si funza wote wa chooni hubadilika kuwa inzi kuna baadhi hufa.
Wale wa vyooni/ wako kwenye hatua ya kuwa nani?Jaim;
Unaposema funza maana yake ni larva stage ya mdudu flan. Hakuna funza wa kudumu kuwa funza. Hawapo na hawatakuwepo
Labda wamejiingiza tu wakajikutiamo kwa nyama ndani ya friji
Wale wa vyooni/ wako kwenye hatua ya kuwa nani?
maembe . unakuta umenunua embe unaona nje zuri ndani ukikata lina funza sasa huyu nzi katua saa ngapi ndani ya embe nijuzeni na hapa.Iron Lady,jibu ni ndio maiti atakayefukiwa na kukingwa kabisa na inzi wasiweze kutaga mayai juu yake basi haitatoa funza(maggots).Si maiti tu hata kwa chakula ama nyama inayooza ikiwa protected vema kutokana na flies haitozalisha funza kamwe.
maembe . unakuta umenunua embe unaona nje zuri ndani ukikata lina funza sasa huyu nzi katua saa ngapi ndani ya embe nijuzeni na hapa.
Fridge yangu pia ina tabia kama hii