Zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wafanya biashara wilayani Simanjiro, mkoani Manyara, linaendelea kwa kutakiwa kutokuwa na wafanya biashara Popo.
Mhandisi Tumaini Magesa, kaimu mkuu wa Wilaya ya Simanjiro akizungumza na wafanya biashara wa Orkesmet na wa mji mdogo wa Mirerani alisema, Serikali haitamani kukutana na mfanya biashara Popo.
Wako ambao wataandikishwa kama wafanya biashara wadogo na wako walioandikishwa na TRA watakuwa na leseni toka kwa Mkurugenzi wa halmashauri, na watakuwa wanalipa mapato TRA.
"Kwa hiyo tunagemea kupata wafanya biashara wa aina mbili ambao ni mfanya biashara mdogo na mkubwa , hatutegemei kupata mfanya biashara aliyekatikati kama Popo" alisema Kaimu Mkuu huyo wa Wilaya ya Simanjiro, Mhandisi Tumaini Magesa.
Alisema Serikali imejipanga kuelimisha wananchi kuhusu elimu ya mlipa kodi ili iweze kufikia malengo tarajiwa.
Akihamasisha wafanya biashara hao (machinga), Katibu Tawala Bi Zuwena Omary alisema, elimu ya mlipa kodi ndio itakayomweka mfanya biashara sehemu salama.
"Usipokuwa na elimu ya mlipa kodi kila kukicha utakuwa unailalamikia Serikali, huku ukipoteza fursa katika nafasi hiyo"
Kuna mbinu nyingi zinazotumiwa kukwepa kodi, nitakuwa mstari wa mbele kuhamasisha wananchi kwa kuwapa elimu ili walipe kodi ya Serikali na sio kukwepa
"Watu wanashindana kukwepa kodi, wakati mataifa mengine yaliyoendelea yanashindana kulipa kodi..hili halikubaliki hata kidogo"alisema Yefred Myenzi Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.
Sent using
Jamii Forums mobile app