Egwugu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,558
- 8,552
Lowassa kutangaza majeshi yetu yako tayari wakati wa sakata la ziwa Nyasa na wakati waziri wa mambo ya nje yupo, wakati waziri wa ulinzi yupo, wakati rais yupo ni jambo amabalo linaongea zaidi na hasa juu ya uwezo wa mhusika. Tena nichukue nafasi hii kumpongeza Membe kuweza kusettle disputes zile na rais Kikwete, kwa Mara ya kwanza naona umuhimu wa vipngozi hawa na inanifanya nijiulize ingelikuwaje Lowasa angelikuwa ndo mkuu wa majeshi ama amiri jeshi mkuu? nchi haiitaji mihemko, Ikulu ni sehemu nyeti ya kufanya maamuzi na ni sehemu ya kuleta maelewano ndani na nje, hatuwezi kuwa na rais wa kusema piga basi watu wanapiga, wakija wahuni wakamwambia piga hao na yeye akapiga itakuwaje? Ikulu hatuwezi kupeleka mtu kama kumpa zawadi, hatuwezi kumpeleka mtu Ikulu kana kwamba tumekosa mtu, urais siyo zawadi wala si harusi, urais ni kazi na kazi inahitaji mtu aliye tayari kiakiri na kimwili nje ya hapo tuachane na kuwaweka watu kama zawadi, kama ni zawadi mpelekeni shopping mkampige viwalo ama mpelekeni tour ili a enjoy ila Ikulu tupeleke wa kufanya kazi zetu na kuheshimu majirani bila mihemko.