Marehemu hawezi kujitetea, ukimlaumu, unamuonea, angekuwa hai angeweza kujibu shutuma, akiwa mfu, unakuwa unajipendelea, maana utabwabwaja peke yako, halafu hatutausikia upande wa pili.
Ndo maana hata wakati wa msiba, sifa nzuri za marehem ndizo hutamkwa.
Mkisema mabaya yake, mnamuonea kwa vile hana nafasi ya kujitetea, maana huenda anasingiziwa.
Mabaya na lawama kwa marehemu humuachia yeye na Mungu wake wamalizane huko!