Pamoja na points zako nzuri mkuu, ulisahau jambo moja zuri; Nini kifanyike?? Tuwape points zetu tu, huenda zikawasaidia hao wenye uwezo. Kama wataisoma hii article, nakuhakikishia kuwa watajua kuwa sasa watu si mazuzu ka walivyoamini.
Si nabii ila, Mimi naona giza nene zaidi kwa Muungano huu. Kama umeshikiliwa kwa gundi ya unga wa ngano vile. Ukikauka, na naona ka tiyari ushakauka waweza katika ghafla.
Viongozi, wamekaa kimyaaaa. Hakuna aliyediriki kutoa tamko rasmi kuhusu uchaguzi. Mnavyozidi kukaa kimya ndo mnavyozidi kuchagiza mihemko. Mngejua mngetangaza pale pale kuwa hakuna mshindi. Sijui, ila nawaza tuu.
Atakaye tangazwa leo, baada ya mda mrefu hivi. Awe awaye au iwe iwavyo, si ni uonevu tuu?? Mkisema uchaguzi urudiwe, si mmewaonea CUF kuwa mbona mlikubali ule wa JMT? Mkisema kuwa Maalim ndo mshindi halali, si mtakuwa mmetaka kumwibia ushindi?? Uaminifu wenyu uko wapi??
Nakuunga mkono mkuu, Uchaguzi huu wa Zanziba, ni zaidi ya tunayo yaona au kuyajua na pia tunayo ambiwa. Taifa la ghilibaaaa. JPM ya Ngoswe mwachiye Ngoswe. Aliyelianzisha yuko mbalii anakuangalia utakavyo limaliza