hashim-shadow of dark destiny!
Hivi vitu viko wazi,kama vazi la kahaba
nasambaza maradhi,alafu nakupa saba
machozi ni haba,uokozi ni njozi baba
ulimwengu wa saba,jehanamu ya aina yake
kipe kitu kikupe,kikutupe kupe kwake
kikunyonye damu kwa hamu
kama hujafaham,dogo mwanaharam
kalamu inamwaga dam
nakuacha mweupe ka'mkologo
chata ka' wagogo
wabongo acheni nyodo,wote mnakula hongo
hivi hii ni serikali,au sera kali kwa mbali,au sera za mali
ni ipi tafakari