Au kwa lugha nyingine, kwa nini ufikishaji ujumbe kwa njia ya mikutano ya hadhara, press conference na mikutano ya kawaida isiwekewe mazingira mazuri zaidi kama njia kuu za ufikishaji habari na maandamano yakawekewe mazingira magumu zaidi kwa kuwa njia hiyo ina hasara kubwa kuliko faida na wakati kundi moja linaitumia, linaathi haki za wengine?[/QUOTE
Habari za jioni kaka, kwa bahati mbaya umezungumza maandamano kwa ujumla. Ulipaswa kusema ni maandamano ya aina gani maana hata makanisani huwa tunaandamana wakati wa ekaristi na huwa tunakuwa bugudha kwa watumiaji wengine wa barabara. Misafara ya viongozi pia huwa bugudha kwa watumiaji wengine wa barabara. Ama kama lengo lako ni kupotosha na kujenga taswira inayojaribu kujengwa na watawala kuhusu maandamano ya wapinzani. Lakini kama kweli una lengo la kuzungumzia maandamano ni lazima ungeshauri maandamano yawe ya amani na kufikisha ujumbe kwa njia ya amani. Nakumbuka enzi za Nyerere kabla ya vyama vingi tulikuwa tunaandama sana kuunga kauli mbiu za wakati huo na hata shughuli zilisimama kwa ajili ya maandamano hayo. Unajua ni kwa nini hali hiyo iliwezekana wakati huo? Ni kwa sababu tulikuwa tunawaza sawa au tulilazimishwa kuwaza sawa. Leo hii waliozoea maandamano ya kuwasifia wamekutana na maandamano yasiyowasifia bali ya tofauti. Kwa hiyo ninachokiona mimi hapo ni ulimbukeni tu wa kukutana na changamoto ya mawazo tofauti na ya kwako.
Hicho ndio ninachokiona kwenye maandamano haswa ya wapinzani especially cdm. Na kwa bahati mbaya ccm wameamua kulitumia jeshi la polisi kuwazuia hao cdm huku wakijua watakaidi na wao watumie kama kete ya wapinzani ni watu wa fujo. Ila nikuhakikishie nchi yoyote inayozuia maandamano ya amani ni lazima itakuwa ama hujenga utawala usiowajibika. Mara nyingi binaadamu ana tabia ya kuwa mtekelezaji bora iwapo anapata mashinikizo, lakini iwapo wananchi wanatumia miziki laini (blues) kuwawajibisha viongozi humo maendeleo mtayasubiri sana.