Hadithi ya kusadikika

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Kutoka kwenye kitabu...

Mbwa aliambiwa: Utalinda nyumba za watu, utakuwa rafiki bora wa mwanadamu, utakula makombo atakayokuachia, na utapewa umri wa miaka 30.

Mbwa akasema: Miaka 30 ni mingi, nataka miaka 15 tu. Akapewa. Hadi sasa huo ndio umri anaoishi mbwa.
Kima aliambiwa: Utarukaruka kutoka tawi hili kwenda lingine. Utakuwa na kazi ya kuwahadaa na kuwachekesha watu. Utaishi miaka 20.
Kima akasema: Miaka 20 ni mingi nataka miaka 10 tu. Akapewa, alijionea huruma.
Punda aliambiwa: Utafanya kazi kuanzia mawio mpaka machweo na kubeba mizigo mizito mgongoni mwako. Utakula shayiri, hutokuwa na akili, na utapewa umri wa miaka 50.
Punda akasema: Nimekubali kuwa punda, lakini miaka 50 ni mingi sana, nataka miaka 20 tu. Akapewa.
Mwanadamu aliambiwa: Wewe utakuwa kiumbe mwenye akili zaidi duniani, utaitumia akili yako kuwaongoza viumbe wengine, utaishi maisha mazuri ili kuiendeleza dunia, na utapewa umri wa miaka 20.
Mwanadamu akasema: Niwe mtu wa kuishi miaka ishirini tu na kila kitu umenipa mimi? Hiyo ni michache mno. Nataka ile miaka 30 aliyoikataa punda, ile 15 aliyoikataa mbwa, ile 10 aliyoikataa kima. Akapewa.
Tangu wakati huo mwanadamu huishi miaka 20 kama mtu, kisha huoa. Baada ya hapo anaishi miaka 30 kama punda, akifanya kazi kuanzia mawio mpaka machweo na kubeba mizigo mizito mgongoni mwake. Watoto wake wanapokuwa wakubwa anaishi miaka 15 kama mbwa akilinda nyumba, kufunga milango na kuzima umeme na kula chakula kidogo au makombo anayoachiwa na watoto wake. Anapozeeka na kustaafu anaishi miaka 10 kama kima. Anahama kutoka nyumba hii kwenda nyingine, na kutoka kwa mtoto mmoja kwenda kwa mwingine. Anatengeneza uongo na visa ili kuwachekesha wajukuu zake.
Kwa nini wafanya kiburi ndugu yangu? Unaujua Mwisho wako?
TAFAKARI
 
Siti ya kwanza mbele kabisa na popcorn zangu.
Mmenisusia ukumbi.....niko mwenyewe
 
Hahahaha who sits down and make these?
 
Iko vizuri mnatamaa ma miaka mingi hamkulifam vyuma .....
 
Hata hivyo umechelewa ile siti ya mbele #1 yenye tvii na kideo, kaiwahi mjanja!
Wewe umekuwa wa mbele, lkn siti ile tamu yenye promisheni, wameikalia wenziyo.
Yaani nimesikitika sana jamani.
Nimeandaa popcorn....kumbe kiti kimekaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…