Wakuu, nimegundua kwanini wabongo tunapigwa gepu na wakenya kwenye soko la ajira. Hatuko serious.
Watu hatufuati maelekezo kabisa. Wengine wanatuma CV in doc format badala ya PDF.
Wengine wanatuma CV pamoja na ma vyeti ya secondary na vyuo.
Wengine hatujui hata namna ya Professional Communications through email.
Mtu ana attach tu CV yake, anatuma. Title ya email haweki, Greetings haweki, supporting explanations haweki....
Wakuu (hasa mliotoka shule muda si mrefu) tusipuuzie maelekezo katika kuomba kazi. Kitu kidogo tu unakua disqualified.