Enyi wadau wa Elimu haya Madodoso ya Kuchangia mawazo ya Grades kwa O-level na A-level manayaelewa?,What is the problem in Tananian Education?is it the Grading system or what else could be the Problem?
Enyi wadau wa Elimu haya Madodoso ya Kuchangia mawazo ya Grades kwa O-level na A-level manayaelewa?,What is the problem in Tananian Education?is it the Grading system or what else could be the Problem?
Wakuu nimetembelea tovuti ya Wizara ya Elimu na kukutana na Dodoso la upangaji wa viwango vya ufaulu. Dodoso la Nimeona wakuu hayo madodoso.
Wizara imeweka mpaka alama 11 mwanafunzi akipata awe amefaulu mtihani wanataka wadau watoe maoni. Mfano wa maswali ni huo hapo
Je, wewe ukiwa kama Mdau wa Elimu unafikiri ni utaratibu gani unaofaa wa upangaji wa Viwango vya Alama za za Mitihani ya K4 na K6 kati ya hizi zilizotajwa? (Weka Alama ya Vema (V) kwenye Kisanduku kilichopo chini ya katika chaguo lako)
UTARATIBU A
A = 81 – 100
B = 61 – 80
C = 41 – 60
D = 21 – 40
F = 0 - 20
UTARATIBU B
A = 80 – 100
B = 65 – 79
C = 50 – 64
D = 35 – 49
F = 0 – 34
UTARATIBU C
A+ = 91 – 100
A = 81 – 90
B+ = 71 - 80
B = 61 - 70
C+ = 51 – 60
C = 41 – 50
D+= 31 – 40
D = 21 – 30
E = 11 – 20
U = 0 – 10
UTARATIBU D
ZOTE HAZIFAI
Alama "U" maana yake ni "Ungraded" na alama hii itatumika kwa wale ambao wameshindwa kupata angalau alama 11.
Kwanza kabisa niipongeze wizara ya elimu kwa kuwashirikisha wadau wa elimu katika kuchangia kuinua elimu yetu inayozorota kila kukicha. Wasiishie kwenye upangaji wa alamu tu, bali waruhusu maoni mengine ya kuinua elimu ya TZ kutoka kwa wadau wa elimu na wanafunzi kwa ujumla wake..
Madani.....
Mimi napendekeza watumie hiyo 'C', kwani itaweza kuonesha kiwango halisi cha ufaulu mtahiniwa....
Swali;
Je utatofautishaje mtahiniwa mwenye A+ flat na mwenye A flat, wakati wote wana overall ya 1:7....?
Jibu;
Hapa nashauri grades zibadilishwe kutoka kwenye rating za mfumo wa division na kuwa katika mfumo wa (A+,A,B+,B,C+,C nk) wakati wa kuasses overall results.