GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,742
- 109,180
mkuu, usiendelee kulisoma hilo gazeti kama ni kero kwako....mimi niliacha kulisoma Uhuru miongo kadhaa iliyopita!Mhariri mwenye akili timamu kabisa hawezi kukubali maandishi kama haya ambayo nayanukuu " Simba SC yafa chali Kifo cha Mende ndembe ndembe ". Matusi haya ya reja reja hayavumiliki na mtasababisha Wana Simba SC wote tususe kununua hiko Kijarida chenu halafu mfe njaa mjini hapa.
Mwisho mwambieni huyo Mhariri wenu Dada Mwani Nyangasa ( kama sijakosea ) ambaye ni Mwana Yanga FC mkubwa arekebishe kuwa Timu hiyo ya Nakuru All Stars siyo ya Daraja la Pili kama alivyoandika leo bali ni Timu / Klabu ya Daraja la Kwanza huko nchini Kenye.
Hilo Dawati lenu la Michezo lilikuwa zuri sana alipokuwa Comrade wangu Dominic Isiji ila kwa huyu Dada yangu Mwani Nyangasa nadhani sasa linapwaya.
Mmetutukana mno Wana Simba SC kwa kutuambia eti chali na ndembe ndembe Kifo cha Mende.
Basi simba hajafa kifo cha mende....chagua ww kichwa cha habari
Waandishi uchwara..!
Mkataa pazuri.... Aone joto ya jiwe au kama sindano ya gentamycine.Unakubaliana na mabadiliko ya minimum requirement- qualification za waandishi wa habari? Nakumbuka kuna kipindi ulipinga sana ile draft ya mabadiliko
Nakumbuka shuleni tulifundishwa kubuni vichwa vya habari.Simba afa Kiume au Simba yaaga Kishujaa au Simba yaachana na Bonanza au Simba ya wapya yasalimu amri.
Hivi ameacha kuvaa viatu ambavyo soli imepinda upande mmoja kama gari yenyr pancha? Niliwahi kufanya field enzi za ujana pale Ila ni moja ya wadada wachangamfu sana sema uYanga wake unani udhi!Tena uchwara kweli Mkuu. Mimi Waandishi wa Habari wenye vinasaba na Yanga FC huwa nawachukia sana Mkuu.