Gazeti la Mtanzania jaribuni kuwa na adabu kidogo kwani mnajidhalilisha Kitaaluma

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,073
107,563
Mhariri mwenye akili timamu kabisa hawezi kukubali maandishi kama haya ambayo nayanukuu " Simba SC yafa chali Kifo cha Mende ndembe ndembe ". Matusi haya ya reja reja hayavumiliki na mtasababisha Wana Simba SC wote tususe kununua hiko Kijarida chenu halafu mfe njaa mjini hapa.

Mwisho mwambieni huyo Mhariri wenu Dada Mwani Nyangasa ( kama sijakosea ) ambaye ni Mwana Yanga FC mkubwa arekebishe kuwa Timu hiyo ya Nakuru All Stars siyo ya Daraja la Pili kama alivyoandika leo bali ni Timu / Klabu ya Daraja la Kwanza huko nchini Kenye.

Hilo Dawati lenu la Michezo lilikuwa zuri sana alipokuwa Comrade wangu Dominic Isiji ila kwa huyu Dada yangu Mwani Nyangasa nadhani sasa linapwaya.

Mmetutukana mno Wana Simba SC kwa kutuambia eti chali na ndembe ndembe Kifo cha Mende.
 
Ni kweli smba kafungwa lakini kwa kilichoandikwa na kigazeti hicho kimetia vhumvi labda kama simba angekuwa amefungwa kuanzia goli tatu kuendelea labda hicho kigazeti kingeleta sense, lakini hapo naona mwandishi katumia mahaba ya sita kwa sita .
 
Kwih kwih kwih
IMG-20170607-WA0018.jpg
 
Mhariri mwenye akili timamu kabisa hawezi kukubali maandishi kama haya ambayo nayanukuu " Simba SC yafa chali Kifo cha Mende ndembe ndembe ". Matusi haya ya reja reja hayavumiliki na mtasababisha Wana Simba SC wote tususe kununua hiko Kijarida chenu halafu mfe njaa mjini hapa.

Mwisho mwambieni huyo Mhariri wenu Dada Mwani Nyangasa ( kama sijakosea ) ambaye ni Mwana Yanga FC mkubwa arekebishe kuwa Timu hiyo ya Nakuru All Stars siyo ya Daraja la Pili kama alivyoandika leo bali ni Timu / Klabu ya Daraja la Kwanza huko nchini Kenye.

Hilo Dawati lenu la Michezo lilikuwa zuri sana alipokuwa Comrade wangu Dominic Isiji ila kwa huyu Dada yangu Mwani Nyangasa nadhani sasa linapwaya.

Mmetutukana mno Wana Simba SC kwa kutuambia eti chali na ndembe ndembe Kifo cha Mende.
mkuu, usiendelee kulisoma hilo gazeti kama ni kero kwako....mimi niliacha kulisoma Uhuru miongo kadhaa iliyopita!
 
Kweli kabisa wangeandika simba yafa kiume ili kuepusha msongo wa mawazo kwa wanasimba ambao bado hawako sawa sana kwa kuukosa ubingwa hapa majuzi wa ligi kuu
 
Unakubaliana na mabadiliko ya minimum requirement- qualification za waandishi wa habari? Nakumbuka kuna kipindi ulipinga sana ile draft ya mabadiliko
Mkataa pazuri.... Aone joto ya jiwe au kama sindano ya gentamycine.
 
Simba afa Kiume au Simba yaaga Kishujaa au Simba yaachana na Bonanza au Simba ya wapya yasalimu amri.
Nakumbuka shuleni tulifundishwa kubuni vichwa vya habari.
Unapewa passage unasoma au shairi au utenzi unaambiwa ANDIKA KICHWA CHA HABARI AU KICHWA CHA USHAIRI.
Kila mwanafunzi aliandika kichwa chake cha habari.
Na tulipata marks sawa.
 
Tena uchwara kweli Mkuu. Mimi Waandishi wa Habari wenye vinasaba na Yanga FC huwa nawachukia sana Mkuu.
Hivi ameacha kuvaa viatu ambavyo soli imepinda upande mmoja kama gari yenyr pancha? Niliwahi kufanya field enzi za ujana pale Ila ni moja ya wadada wachangamfu sana sema uYanga wake unani udhi!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom