Dah, hujawahi kuchange ATF ever since? Hebu kafanye service kubwa, weka plug mpya original za toyota, weka ATF ya BP, badilisha Aircleaner, engine oil.. Lakini pia inategemea na ODO inasoma ngapi hapo kwenye Dashboard, mara nyingi gari ndogo engine ikashavuka 160,000km engine perfomance inapungua especially kwa matumizi ya hapa kwetu, ATF usiwe unaiacha Muda mrefu hivyo.
Ikiwa kama unampa tu fundi,basi kuna sehemu au kuna kitu ameweka ambacho sio sahihi, ndio maana unaona gari yako imeanza kuleta usumbufu!thanks wakuu, kwenye ishu ya Oil na ATF niende sheli za Total au BP kwa engine hii?
Na Plugs original za Toyota kwa Dar nazipata wapi? Maana nimezoea nampa gari tu fundi anachange Oil na Oil Filter baadae analirudisha. So sijui ata anawekaga BP au Total. Nilikua mzembe kidogo hapa.
Wow,Mkuu this time fanya service mwenyewe ukiwa unaona mafundi watakuwekea oil cheap utaua gari then badili oil ya gear box na air cleaner gari itakaa sawa oil weka ya bp 75000
Ikiwa kama unampa tu fundi,basi kuna sehemu au kuna kitu ameweka ambacho sio sahihi, ndio maana unaona gari yako imeanza kuleta usumbufu!
Usiamini sana fundi. Jaribu kuwa makini na chombo chako. Kama huna muda ni heri uipaki, utumie public transport then ukipata muda ndio uende garage.
Lakini sio tu kumuachia fundi aende nalo, wengi magari yao yamechangiwa sana kuharibiwa na mafundi.
Kuna garage iko kamata, naona ni ya kisasa, waweza kwenda gari yako wakaifanyia vipimo kwanza A to Z.
Hii mambo ya kukisia kisia bila gari kufanyiwa vipimo, siipendekezi sana, maana waweza jikuta mnabadiki vitu ambavyo ni vizima mkidhani kuwa ni vibovu!
Huo ndio ushauri wangu!