Kwanza mtu una machungu ya kusota na elimu yetu ngumu, ukisha pata kazi unataka ujifariji kidogo na uonyeshe watu kwamba umeanza kula matunda ya taabu yako (gari utatembea nayo na kila mtu atakuona lakini nyumba sio kila mtu utakaekutana nae atajua kwamba unamiliki nyumba)
Pili wengi tunaamini kujenga kunahitaji kua na pesa nyingi sana na zile tunazopata kwa mwezi tunaona kama haziwezi kufanya kitu kwenye ujenzi kumbe tunajidanganya.
Mwisho ni vipaumbele vya mtu binafsi na amechagua nini kwenye maisha yake. kuna mwingine yuko tayari apane nyumba ya sh. 600,000 au zaidi kwa mwezi ilimradi aishi eneo analolipenda wakati kuna mwingine yuko tayari amiliki nyumba yake hata kama ni mbali kiasi gani.