G.Lema kuzuru kaburi la Baba wa Taifa

Earthmover

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
26,012
Reaction score
25,353


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), anatarajia kuzuru Butiama, mkoani Mara kwa ajili ya kutoa shukrani katika kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.



Lema amefikia hatua hiyo baada ya Mahakama ya Rufaa kumrudishia ubunge wake.Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere, alisema ziara hiyo inatarajiwa kufanyika baada ya msimu wa sikukuu kwisha.



Nyerere alisema Lema atakwenda kutoa shukurani, kwani awali aliponyang’anywa ubunge alikwenda kuomba haki itendeke katika rufaa.


“Tunakwenda na Lema katika kaburi la Baba wa Taifa, amesema anataka kwenda kutoa shukrani baada ya kupata ubunge wake alionyang’anywa na mahakama. Unajua hapo awali alikwenda Butiama katika kaburi na kuomba atendewe haki na kweli haki imetendeka,” alisema Nyerere.


Nyerere pia alisema kuwa baada ya kutoka Butiama watafanya ziara katika Mkoa wote wa Mara yenye lengo la kuhakikisha wanawavua wananchi magamba na kuwavalisha magwanda.Alisema katika ziara hiyo watatoa elimu na kutangaza sera ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi wa wenyeviti wa serikali za mitaa.


Akizungumzia ziara yake aliyoifanya Kasamwa, Kakolwa, Kyela, Iringa na Tunduma, alisema kuwa ilikuwa na mafanikio makubwa.



source: Tanzania daima 27 December 2012

My Take:

....chadema imemjenga G.Lema na huku ndiko anakoelea.....

....Charismatic Leaders are often thought of as heroes that are able to use their personal allure to lead others. But that charismatic charm can be both a blessing and a curse on society. That's because charisma can be used for the good of a company or nation - but also for less-than-honorable reasons......
 
mmh! haki itendeke? kumbe ndio maana majaji wakatoa hukumu based on their own theories ambazo hadi sasa zimeacha maswali vichwani mwa watu sio??
 
Hivi ameshakuwa Mt tayari? Wakati anaomba, akiomba Mwl amuombee, kama hivyo ndivyo basi itawekwa kwenye record kuwa Mwl aliinterviene for him.

Haya mambo ya kutoa heshima au kuomba kwenye makaburi yanahitaji umakini wa hali ya juu.
 
Hivi ameshakuwa Mt tayari? Wakati anaomba, akiomba Mwl amuombee, kama hivyo ndivyo basi itawekwa kwenye record kuwa Mwl aliinterviene for him.

Haya mambo ya kutoa heshima au kuomba kwenye makaburi yanahitaji umakini wa hali ya juu.

Kweli kweli
 

Nyerere alisema Lema atakwenda kutoa shukurani, kwani awali aliponyang'anywa ubunge alikwenda kuomba haki itendeke katika rufaa.

Kuna thread nilichangia wakati lema anajibu taarifa ya JWTZ nikasema watu wanaomshirikiasha Mungu uwa ni level nyingine kabisa.Kwa sisi wakristu uwa kuna imani ambayo ukiifanya na kuifuata kama vile kufunga na kusali Mungu ujibu maombi yako!!!Yeye lema kwa hili alipeleka imani yanke huko na hakika imejibu sasa wale wasio amini waendelee kutoamini wasubilie mtiti wake, hsa mtu mweye imani ya aina hii anapoitafuta haki uwa hazuiliki.Ukitaka kujua haya mambo ni mazito kiaje katafute kaburi la Hitler, Mobutu, Osama au Sadam kisha ukiyapata njoo hapa tuzungumzie!!!

Kwa kuwa kafanikiwa na kilio chake kimesikilizwa basi ni vyema aludi kutoa shukrani kitu ambacho ni sahihi,ombi langu kwa wasio kuwa na imani,kama kweli imani ya Godbless lema ndiyo hii,hakika nawapa pole wengi sana ambao hawajui haki kwa wengi nini?

Mdau kama unamuweka G.Lema kwenye kundi la charismatic Leaders umekosea sana ,huko hayuko,kwa ishara hiyo juu huyu jamaa anaendesha mambo yake kwa hofu ya Mungu,kitu ambacho kama anaijua haki ni hii,uwezi kumpindisha hata kidogo,zaidi atakutia matatizoni ili haki anayotafuta itimie.
 
.....ha ha ha magamba wanataka kutoa tamko.....
 


MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA), anatarajia kuzuru Butiama, mkoani Mara kwa ajili ya kutoa shukrani katika kaburi la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

.

Kwani wakristo huwa wanaomba wafu makaburini badala ya mungu?
 
Go Lema, huyu baba yetu wa Taifa angekuwa na uwezo akifufuka akiona hali ilivyo Tanzaniakwa sasa ataomba afe na asifufuke tena milele!!
 
Hivi ameshakuwa Mt tayari? Wakati anaomba, akiomba Mwl amuombee, kama hivyo ndivyo basi itawekwa kwenye record kuwa Mwl aliinterviene for him.

Haya mambo ya kutoa heshima au kuomba kwenye makaburi yanahitaji umakini wa hali ya juu.

WAKUBWA MMEANZA KUABUDU MIZIMU SASA MAANA NINAVYOWAFAHAMU NA IMANI ZENU HABA,SASA HIVI MTAJENGA SANAMU LAKE KWENYE MAKAO MAKUU YENU MUANZE KULIABUDU.SHAME ON YOU!NA KUJITIA USOMI WOTE BADO MNAABUDU WAFU?:flock:
 
Hivi kwa kuabudu kwenu wafu ndo mnataka kuongoza nchi?mshindwe kabisa!
 
Nyie mbezeni tu Lema lakini Spirit aliyonayo kupigania haki anawazidi Wanasiasa karibia wote.Watanzania wanataka mtu wa namna hii mwenye moyo wa kipiganaji.

Wanamapinduzi wengi wanamioyo ya hivi na walibezwa sana kwa elimu zao na kila aina ya matusi lakini mwisho waliaminiwa na umma na kuongoza mapinduzi!

Mbezeni Lema lakini ushawishi wake unajambo la ziada linalotamaniwa na wengi!
 
Reactions: DSN
Kuna kiongozi mmoja mkristo alikumbana na mtiti kweli kweli ,kuw mbona ajaonekana kwenye kaburi la Baba wa Taifa kulikoni!!!Hatimae yule Mheshimiwa anajua kuwa alikuwa ajajipanga akaipanga akazuka eneo lile,lakini alienda baada ya mashinikizo mengi huku n huku.Lakini huyu anaekwenda huko kwa kusukumwa na hiari na kuona ni sehumu sahihi ya kwenda kama unavyosema waendelee kumbeza siku ya siku watashangaa kinachofuata.

Watanzania wakizidi na mambo kama migogolo mashuleni, vyuoni, maofsini, viwandani, uwa na namna ya sara yao ya kufika kaburini Butiama kwa baba wa taifa,toka pale walipo kwa njia ya Spirit bila kujali dhehebu wa dini gani mtu anatoka.Yani ndio kusema watanzania wale usafri kwa umoja kwa njia ya spirit mpaka butiama na kuongea na Mwalimu kwa namna ambayo wengine uona kama ni wimbo lakini kumbe ndio sala yenyewe hiyo..

Wimbo wenyewe huwa ni huu " Kama sio juhudi zako Nyerere X 2 Na .............. angesoma wapi?" ebu pata picha anaetajwa ni as if yuko hai-ebu angalia sentensi hiii -kama sio juhudi zako Nyerere.Ni sentensi ambayo inaonyesha mtajwa yupo anaishi.Je ni kweli bado Mwalimu tunae,au ndio zile sentensi za lema na kina stev Biko wa South Africa.Na nina amini kwa dhati kuwa wazee wengi wa CCM, na walio serikali walisoma sana vitabu vya wapigania uhuru kama kina Stev biko, Olver Tambo, Sisuru na kwa Marekani walimsoma sana Martin Luther King Junior, na ndoto yake kubwa ya I have a dream.

Obama amekuwa Rais wa Marekani kutokana na ndoto ya Baba yake,Watu wazima wengi weye umri wa Baba yake Obama wanajua dreams za Barak Obama Senior, alikuwa ni mchumi wa aina yake East Africa.lakini kwa siasa za Kenya za ukabila nafasi ya dream yake iliperish na yeye mwenyewe kwa stress.Lakini mtoto aliiona machaoni mwa baba yake na leo hii katimiza sio kwa kuitawala Kenya bali kwa kutawala Taifa kubwa duniani,and soon ile ndoto iliyokuwa aiwezekani kuwa jaluo anaweza kuwa Rais wa Kenya basi ndiyo iyo ishapiga hodi wanachosublia ni kuvuta vigoda vya Ikulu.

Hakika kuzalau watu aina ya lema da nawapa pole wasio jua miujiza ya Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…