G-7 kupambana na China

DENG XIAOPING

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2022
Posts
2,392
Reaction score
2,599
- Mataifa Saba yaliyo na nguvu za kiviwanda na kiuchumi maarufu Kama G-7 [ United States of America, England, Germany, France, Italy, Japan and Cannada ].





- Yamefikiana makubaliano ya pamoja ya kuwekeza zaidi ya fedha za kimarekani dollar billion 600 kupambana na mradi wa china Belt and Road Initiative ulioanzishwa na China Mwaka 2013 ambapo china iliwekeza zaidi ya dollar Trillion moja [ 1T dollar ].




- Mradi wa China wa Belt and Road Initiative ulianzishwa na Serikali ya China 2013 . Lilikuwa ni wazo la Rais wa Sasa wa China bwana Xi Jinping kabla ya kuwa Rais kuanzisha mradi utakao iunganisha China na duniani kupitia miundombinu ya reli , barabara , kwa njia ya maji pamoja na kwa njia ya anga ili dunia iweze kunufaika na China na China kunufaika na duniani kupitia biashara pamoja na sayansi na teknolojia. Baada ya kuwa Rais mwaka 2013 wazo lake lilipitishwa na serikali ya china na kuwa mpango wa serikali ya China ambapo serikali ya china iliwekeza zaidi ya dollar Trillion moja [ 1T dollar] kwa mradi wote.




- Belt and Road Initiative uweza kuwapatia mikopo ya kimaendeleo nchi washirika ili kufanikisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo mfano ujenzi wa barabara , reli , viwanja vya ndege , bandari n.k

- Pia umoja wa mataifa yenye nguvu kubwa duniani kiviwanda na kiuchumi maarufu Kama G-7 wamekubaliana kwa pamoja kuwekeza zaidi ya dollar billion 600 kuzisaidia nchi masikini zinazoendelea [ Africa , Latin America n.k ] kimikopo ili kuweza kufanikisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.





- Ambapo ndani ya uwekezaji huo Marekani pekee imechangia zaidi ya dollar billion 200.



- Mwisho ni nini maoni yako juu ya mpambano huo mkali kati ya project ya G- 7 yenye thamani ya dollar billion 600[ 600B usd ] na project ya china ya Belt and Road Initiative yenye thamani ya dollar Trillion moja[ 1T usd ]?
 
Halafu anatokea mtu mmoja huko mbagara anasema China si lilote si chochote wakati ni one manshow vs many.
 
Mchina yuko juu, yaani amewashinda mawazp mataifa saba?
 
Mbona hakuna mpambano hapo zaidi kwamba wote ni wasaka fursa. Ni kama wewe unavyoamua kulima mahindi zaidi ili umzidi wa shamba la jirani. Africa tungeweza kua na uwezo mkubwa wa teknolojia na uzalishaji wa bidhaa na huduma basi hawa mabwana wangetulia
 
Naam nguvu ya ziada inahitajika ili tuweze kujikwamua kisiasa,kiuchumi,kijeshi,kisayansi na teknolojia
Nalog off Z
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…