Fursa Dodoma

Jirambe

Member
Joined
Apr 12, 2019
Posts
7
Reaction score
13
Habari wana JamiiForums,

Nimehamia kikazi kutoka Dar sasa nipo Dodoma.Nina wiki ya pili sasa na zifuatazo ni chamgamoto ambazo ndio fursa za biashara Dodoma mjini..
1.Kunyoa nywele sh 3000-fursa-ukifungua barbershop yako ya kawaida ukanyoa kwa 2000 utapiga hela coz sio wote wana afford bei hiyo..pia barbershop ni chache sana

2.Biashara ya mgahawa-huku wali nyama 2500-3000..wali maharagwe 1500-2000..hiyo ni fursa

3.Kampuni ya usafi-watu wengi wa huku especially wafanyakazi wanapenda kufanyiwa usafi, hata hapa nilikopanga nimeambiwa kila mpangaji anachangia 6000 ya usafi kwa mwezi...usafi unaofanywa(chooni na bafuni+baraza+kumwaga taka)..pia hakuna kampuni nyingi za usafi compare to Dar..

Hizo ni fursa chache kati ya nyingi nilizoziona hapa Dodoma. Mnaweza kuongezea pia kuzifanyia kazi kujikwamua na umaskini.

''EAT WITH YOUR FRIENDS DON'T COMPETE WITH THEM..THE HUSTLE IS AGAINST POVERTY NOT FRIENDSHIP''
 
Fursa niliyoiona ni hiyo namba tatu. Umejaribu kupita madukani ukaona mchele, maharage, nyama inauzwa bei gani? Pia nasikia Dodoma maisha yapo juu, ni rahisi kutengeneza elfu kumi kwa siku lakini ni rahisi pia hiyo elfu kumi kuisha kwa siku. Haya ni maneno ya wananzengo sio yangu
 
Ni kweli maisha yapo juu sana...unajua kama rahis kutengeneza pesa kinachokwamisha wengi kuendelea ni nidham ya kuitunza hiyo pesa ili izunguke zaid kwenye biashara na sio kuitumia kwenye kitu ambacho hakiingiz pesa
 
Hata uwe na nidhamu kuna mambo hayakwepeki. Utaacha kununua mboga? Utaacha kununua maji?

Ndugu ukisema hivyo utashindwa kufanya biashara maana kila sehem changamoto hizo zipo..ni wewe tu jinsi gani utavyojipanga na ili ufanikiwe lazima uwe na multiple sources of income otherwise popote utaona pagumu
 
Ni kweli mkuu

Garage za maaana ni chache sana na wengi wananyodo sana kama kina nduvini au yule muhindi wa Action pale.
 
Garage za maaana ni chache sana na wengi wananyodo sana kama kina nduvini au yule muhindi wa Action pale.
Yes mkuu sasa hizo ndo fursa kama wanaringa inabid utumie mwanya huo huo kupiga hela yaan ww uwe humble kwa customer wako
 
Fursa
namba tatu nitaifanyia kazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…