FUNDO LA KUZIMU (shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1>kwanza iandae kucha,usinyonge unyayoni.
Mchana usiku kucha,zitazame vidoleni.
Na vaa vazi la bucha,kwa nje siyo moyoni.
Fusho vundo la kuzimu,lifukize kwa mashuke.
2>baraza limeshakucha,vibaraka kikaoni.
Gongo supu ya mchicha,isopikiwa jamvini.
Siri iliyojificha,inafuka hadharani.
Fusho vundo la kuzimu,lifukize kwa mashuke.
3>akili waipikicha,imani haba nyoyoni.
Umejenga mbaya picha,huaminiki mtani.
Umekufa wako ucha,jiandae kifungoni.
Fusho vundo la kuzimu,lifukize kwa mashuke.
4>bora tabia kuacha,usifike matatani.
Ukweli umejificha,ndani ya shimo rohoni.
Ni chakula kimechacha,kula kigande tumboni.
Fusho vundo la kuzimu,lifukize kwa mashuke.
5>tena ufikiri kisha,tafakari kwa makini.
Tufe uliwezi rusha,bila dole mkononi.
Mwenyewe wajiangusha,wajitia hasarani.
Fusho vundo la kuzimu,lifukize kwa mash
uke.
Shairi=VUNDO LA KUZIMU.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 au 0655519736
 
tisha bovu!....lakini mkuu dhima kubwa ya shairi lako ni nini haswa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…