Nashukuru mkuu kwa taarifa nzuri tulikuwa wote jana pale uwanjani na nilikuwa naona vijana wetu wa msimbazi wakitandaza soka la kimataifa zaidi ila nikurekebishe tu mkuu pale jana jonasi mkude hakwepo ni mgonjwa ila leo tunatarajia kumuona kionga bora kabisq ukanda huu wa afrika mashariki na kati si mungne ni Haruna moshi boban atakwepo leo tutakuwa pamoja mwanzo mwisho wa mtanange SIMBA NGUVU MOJA
Mkuu labda itakua ni mtandao tu.. Ila zinafunguka.
Wimbi la ushindi la simba sc linaendelea bado na leo tumetoa dozi ya goli mbili bila majibu kwa polisi ya zanzibar magoli yakifungwa na Mussa mgosi kipindi cha kwanza na Elias manguli kipindi cha pili na mpaka dk90 refa anamaliza mtanange simba 2 polisi 0 pia tumeshuhudia kiungo machachari kabisa mwinyi kazimoto akiwa na klabu yake ya zamani ya simba tayari kujiandaa na mazoezi natumaini jumatatu ktk mechi ya kirafiki atakwepo uwanjani
asante mkuu kwa kutujuza Simba chama kubwa
Asante kwa taarifa
Mkuu hizo ni tetesi.. Tuwe wavumilivu, na tuombe isitokee.
Jana simba ilicheza mechi yake ya tano ya kirafiki na kuifanya vizuri tena kwa mara ya tano ushindi mfululizo kwa kushinda goli 3 dhidi ya 2 za KMKM ikicheza mpira mzuri zaidi na wa kisasa zaidi uwanjani huku mashabiki wakishangilia sana