Membe anatangaza nia take juma2 mkoani Lindi. Tayari maandalizi yameshafanyika. Hafla hiyo ya kutangaza nia ilikuwa ifanyike J1 lakini imesogezwa mpaka tarahe 7.6.2015.
Inavyoonekana mwaka huu ili kupunguza makali ya chama kusambaratika baada ya uteuzi Wa mgombea, huwenda wale wote waliosimamishwa miezi 12 kwa kuanza kampeni mapema safari zao zikaishia kwenye vikao vya awali!
Huenda pia wimbi kubwa la wanachama wengi wa CCM kutangaza nia ni mkakati uliyosukwa vizuri, ili kuwakabili baadhi ya makada wenye nguvu ndani ya chama.
Hii Ina maana kwamba wakienguliwa wengi wale wakose hoja za kulalamika. Hata hivyo wadadisi Wa masuala ya kisiasa wanashauri kuwa, mbinu inayotakiwa kutumika itakiacha CCM hoi na vipandevipande.
"Ni bora wakawasikiliza wananchi wanamtaka nani, matokeo ya kura za maoni, ya vijana waliotumwa mikoani na Chama ingetumika kumpitisha mgombea anayekubalika" alisema mchambuzi mmoja wa kisiasa. Aliongeza kuwa " Kizazi cha Leo hakifahamu CCM, wengine wamekuwa wakati chama hiki hakina nguvu na upizani una nguvu, kwa hali hii, haijalishi ni mtume au malaika atateuliwa na Chama. Muhimu kupitia yote ni mtu ambaye Watanzania wenyewe wanayemtaka, hiyo ndiyo itakayokuwa salama ya chama".