Zamani kutoka buguruni kwenda tabata kulikua na foleni sana, lakini polisi wa kituo tabata angalau walisaidia waliporuhusu service road kutoka matumbi kwenda tabata itumiwe pia na dalada, foleni ikapungua sana.
Sasa polisi wa bugurini nahisi ndio wanaohusika kwani nini hawaruhusu njia ya sukita - buguruni rozana itumike?
Foleni ingepungua sana maana daladala zote zinazokuja mnazi mmoja zingetumia njia hiyo kuwahisha abiria kazini.
Daladala zisingelazimika kupitia buguruni mataa kwenye foleni.
Magari yanatumia mafuta mengi kwa ajili ya foleni, abiria nao ili wawahi kazini wanalimika kushuka na kupanda bodaboda ili wawahi kazini, inaumiza sana kimapato napia mda mwingi kukaa kwenye foleni ambayo ingeweza kuepukika.
Tunawaomba wahusika jamani watutatulie haza hii.