Fighting for Tanzania

Genius Man

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2024
Posts
3,559
Reaction score
7,914
Fighting for Tanzania

"Fighting for Tanzania" ni nini ?

ni uhamasishaji wa mabadiliko chanya kwenye nchi na kupinga vikali matukio ya kiuhalifu na utekaji, matukio yote ya uvunjifu wa haki za binadamu, matukio yote ya matumizi mabaya ya madaraka, matukio yote ya ukiukwaji wa makusudi wa katiba ya nchi, matukio yote ya chaguzi sizizo za haki, matukio yote ya ubaguzi wa rangi, matukio yote ya ubaguzi wa uraia wa afrika mashariki na duniani kote, matukio yote ya kutumia vibaya rasilimali za nchi.

Fighting for Tanzania, ni uhamasishaji wa mabadiliko chanya na sio vurugu, au kuchoma moto ikulu au kituo cha polisi, au kumteka raisi, au aina yoyote ya uhalifu.

Fighting for Tanzania itaisha pale mabadiliko yatako fanyika kwenye nchi na kurudisha utawala wa vitendo wa haki ya kweli na demokrasia na sio mdomo pasipo ubaguzi wowote au aina yoyote isiyofaa.

Natumia uhamasishaji huu kuunga mkono mabadiliko na kuwaunga mkono wote walio tekwa na damu zilizo mwagika katika kupinga mambo yote maovu Tanzania, naunga mkono wapigania haki wanao shikiriwa kwa sababu ya kupigania haki na mabadiliko, naunga mkono wale wote walio pewa ulemavu kwa sababu ya kulipigani taifa.

Naunga mkono haki za wale wote ikiwemo wakenya waliobaguliwa na mamlaka ya Tanzania kutoingia.nchini pasipo kuwa na hatia yoyote au kosa lolote kisheria.

Nahamasisha watanzania kwa hiyari yako weka hii picha ya "Fighting for Tanzania" hapo juu kwenye profile yako kuonesha mshikamano wako kwenye kuhamasisha mabadiliko chanya kwenye taifa bila itikadi za kivyama wala kidini.

Weka hiyo picha kuunga mkono wale wote ambao damu zao zimemwagika kwaajili ya Tanzania, weka kuunga mkono wale wote walio shikiriwa kwa kulipigania taifa na kuongea ukweli bila kujali, weka kwaajili ya kuunga mkono mabadiliko ya kiuchaguzi, weka kwa kuunga mkono wale wotewaliobaguliwa na mamlaka ya Tanzania kuingia nchini.

ukishaweka comment hapo chini "FIGHTING FOR TANZANIA" wewe ni shujaa.
 
Mikakati ni ipi?

NRNE lazima iwe na mikakati, vinginevyo imefeli kabla ya kuanza.
 
Mikakati ni ipi?

NRNE lazima iwe na mikakati, vinginevyo imefeli kabla ya kuanza.
Weka picha kuunga mkono mabadiliko chanya kwenye taifa hili ndio lengo tunataka mabadiliko, uungaji mkono uhamasishaji huu utachochea mabadiliko nchini.
 
Weka picha kuunga mkono mabadiliko chanya kwenye taifa hili ndio lengo tunataka mabadiliko, uungaji mkono uhamasishaji huu utachochea mabadiliko nchini.
Mabadiliko yepi makhususi? Maana listi yote inaweza kuanzia hapa hadi Alpha Centauri.
 
Wasambazie member wengine waweke kwanza tuwe wengi kwanza hapa JF kisha tuingie sehemu ya pili
Mijadala isiyo na active, realistic actions ni kujichosha bure.

Afadhali Sidiemu wameamua kuchukua hatua ya kutopiga kura.

Tunaweza kuwapongeza kwa hilo, japo utekelezaji wake lazima wawepo watu na nusu wanaojua wanalofanya.
 
wazo zuri, Mabadiliko yanahitaji shinikizo na sio kwa kutegemea kitu kimoja hayatukuwa rahisi weka picha kuunga mkono mabadiliko
 
wazo zuri, Mabadiliko yanahitaji shinikizo na sio kwa kutegemea kitu kimoja hayatukuwa rahisi weka picha kuunga mkono mabadiliko
Mkuu, hakuna mtu asiyependa mabadiliko.

Sema tu kwamba watu wengi wanaona gharama ya mabadiliko ni kubwa mno, kwa hiyo wanachagua status quo.
 
Naunga mkono juhudi zozote zenye kutuletea mabadiliko dhidi ya mifumo hii ya KIIMLA inayong'ang'aniwa na CCM.
Sisiemu wao wanasema kazi imefanyika almost 100% kiasi kwamba Sidiemu imekosa hoja, ndiyo maana inataka kubadili kanuni za mchezo ili ipewe ushindi wa mezani.
 
Mkuu, hakuna mtu asiyependa mabadiliko.

Sema tu kwamba watu wengi wanaona gharama ya mabadiliko ni kubwa mno, kwa hiyo wanachagua status quo.
Hii ni kwa mashujaa kama wewe muoga usiweke lakini kuunga mkono mabadiliko usiache
 
Hii ni kwa mashujaa kama wewe muoga usiweke lakini kuunga mkono mabadiliko usiache
Mkuu, unaambiwa uoga ndiyo akili.

Hata TAL anaogopa, japo ameamua kuuvaa ujasiri usio wa sayari hii.

Kuna siku alihojiwa kuhusu kukimbilia Ubelgiji 2020 baada ya uchaguzi, akasema: ^Lazima niishi ili niweze kupambana siku nyingine!^
 
Sisiemu wao wanasema kazi imefanyika almost 100% kiasi kwamba Sidiemu imekosa hoja, ndiyo maana inataka kubadili kanuni za mchezo ili ipewe ushindi wa mezani.
CCM wao hawataki Reforms za Katiba na Sheria za uchaguzi kwasababu wanataka mfumo huu wa KIIMLA uendelee ili wabakie madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…