Kwanza nipongeze hili wazo la kuanza kusherehekea urithi(utamaduni) wetu kila mwaka ambapo kwa mwaka huu litaanzia Dodoma kesho tarehe 15/09/2018. Kuna tatizo naliona hapa hasa kwenye jina la tukio lenyewe hasa kwenye neno "festival" [emoji20] [emoji19] hivi mnataka kutuambia hamna neno la kiswahili ambalo lingeweza kukaa hapo badala ya hilo neno la lugha ya wakoloni?! Ni kipi hasa cha kujivunia urithi wetu kama hata jina tu tunaweka lugha ya kigeni ambayo sio urithi wetu?! Nashauri neno "festival" liondolewe ikiwezekana iwe "Urithi Wetu" au "Urithi wa Nyumbani" n.k