Ili tangazo liitwe tangazo bora la biashara hasa humu mtandaoni inabidi liwe na mambo haya
1. Bei halisi ya bidhaa yako (isiwe kubwa zaidi ya ile ya dukani kama bidhaa ni used na isiwe sawa na ile ya dukani. Km unataka kuuza kweli) baada ya kuweka bei yako ongeza na neno maelewano yanaruhusiwa.
2. Mahali ilipo bidhaa. Hata km kabati/sofa utauza elfu10 lakini likiwepo Marekani bado ni ghali tu
3. Picha za bidhaa. Hii itasaidia wadau watathmini ubora wa bidhaa kulingana na gharama uliyoweka.
4. Mawasiliano. Hakikisha namba unayotoa iwe active 24/7.
Mengineyo wataongezea wadau