Nakushauri totolesha vifaranga. hautapata faida kwa kuuza mayai zaidi ya hasara siku ukipiga hesabu ya garama utawauza. mi nilianza rasimi ufugaji na jike 10 na jogoo 1 mwakajana mwezi wa 8. sasa ninao kuku 120. vifaranga 60 walio atamia wapo 6
nilicho kifanya nilikuwa nikiatamiza mf. kuku 6 wakitotoa kuku 3 wanalea. 3 naziwekea mayai mengine toka kwa wafugaji wengine. trei 9,000 nilhkuwa napata vifaranga 20 -25. usinunue mayai ya sokoni mengi yamepita mda wake yasizid siku 14 toka kutagwa,
kulea vifaranga wala si tatizo. kwahao kuku wako banda la bati 3 za mita 3 au 2.5 litakutosha. PM namba yako nikuelekeze cha kufanya dhidi ya vifaranga na kama utakuwa karibu na nilipo naweza kukutumia kitabu (bule) bila malipo nilicho toa SUA
Nakushauri totolesha vifaranga. hautapata faida kwa kuuza mayai zaidi ya hasara siku ukipiga hesabu ya garama utawauza. mi nilianza rasimi ufugaji na jike 10 na jogoo 1 mwakajana mwezi wa 8. sasa ninao kuku 120. vifaranga 60 walio atamia wapo 6
Strategy nzuri!,hongera sana mkuu!
asante kiongozi wangu. malengo yangu. mwaka kesho mwezi kama huu niwe nimezarisha na kuuza kuku 3,000. naomba Mungu ilmalengo yangu yatimie.
Habari Wadau wenzangu!
Nina siku 15 (Wki 2 nasiku 1) tokea nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji. Nilianza na Majike 15 na jogoo 1, nashukuru leo tarehe 21/09/2014 nimekamilisha trei moja la mayai na kupata mteja mara moja (Inaonyesha biasara ya mayai ya kuku wa kienyeji ni nzuri kuwa yana hitajika kwa wingi).
Plani yangu Mpaka mwisho wa mezi huu ninunue mitetea 10 mingie na jogoo 1 jumla ya uku wote iwe 27, ili niongeze uzalshaji wa mayai. Na kufikia mwezi wa 11 ninunue eneo kubwa la kufugia kibiashara maana hapa ni kama natafuta uzoefu.
Kimenistua kitu kimoja niliona juzi Mtetea mmoja una chechemea nikamshika baada ya kumchunguza nikamkuta anakidonda chini ya nyayo zake (Kama inavyo onekana kwenye picha ya tatu hako kakidonda kanjano hivi) kwa sasa hali yake si mbaya yupo karibu kurecover.
Naomba ushari juu ya hili tatizo la huyu mtetea ili niweze kulikabili lisiudie tena maana nahisi hajisiki vizuri na anaweza punguza utagaji.
Nashukuru wadau wote walio nihamasisha kuingia kwenye ufuaji kwa amna Tofauti tofauti.
Wenu katika UJASIRIAMALI: pH 7
kama unafikiria kutotolesha, idadi ya matetea isizidi kumi kwa kila jogoo ili kupata mayai yaliyo chavulishwa vema.
Shukrani Mkuu, Kwa sasa ninalo jogoo moja sababu idadi ya mitetea yenye uwezo wa kutaga haizidi kumi. Ila nimejipanga kuongeza majogoo yawe angalau mawili wakati wa kuongeza mitetea.