Fao la kujitoa nssf

mfianchi

Platinum Member
Joined
Jul 1, 2009
Posts
12,337
Reaction score
9,299
Wadau naulizia kuhusu sheria inayohusu fao la kujitoa kwa mwanachama wa NSSF,je bado hilo fao lipo ?na je mwanachama bado unatakiwa kusubiri hadi miezi sita ndio upate hilo fao?je ni kipengere kipi kama kipo kinaruhusiwa mtu kuchakua fao mara tu uachapo kazi ?
 
Chelewa chelewa mwana utakuta si wako! wenzio tunasubiri cheque tu.
 
Mi sijaelewa logic ya kusubiri miezi sita, baada ya kuacha kazi naomba ufafanuzi
 
Mi sijaelewa logic ya kusubiri miezi sita, baada ya kuacha kazi naomba ufafanuzi

Katika nchi yetu ukianza kufuatilia kuhusiana na logic unaweza ukafa kwa kichaa, hakuna logic hata kidogo ni kikundi cha watu tu walikaa wakaamua eti ukae miezi sita ukisubiri hela yako. Walitaka ndani ya miezi sita ufe kwa frustration ili wao ndo wazile hizo hela
 
Tena wanaamua wakiwa kwenye vijiwe vyao wanapokutana kama vile Gymkhana,British Legion.karibu na soko la samaki ferry
 
Loo bado hakuna jibu kuhusu hilo fao
 

Sekta ya madini ruksa kufungua mara tu kazi ikiota. Sekta nyingine bado wana sheria ya kusubiri ezi 6
 
Miezi 6 kwa sababu kuna wanao acha kazi na kuajiriwa sehemu nyingine na hivyo kuendelea kuwa mwanachama wa mifuko hii ya hifadhi ya jamii.
Sekta ya madini moja kwa moja kwa kuwa wafanyakazi wa sekta husika hupata madhara ya kiafya na pia kutokana na makubaliano yaliyofikiwa kati ya sekta husika na mifuko.

Hatahivyo;
hakuna logic kwa sababu mwenye kuamua kuendelea kuajiriwa au vinginevyo ni mwanachama wa mfuko husika.
 
Hata wao wanakigugumizi kuhusu mwisho wa ishu hii maana nzito. Hamna anayetaka kujitoa kafara kama Madam Irene...kwa hiyo lets enjoy for now, tuchukue hela yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…