Familia ya Jitambue Popote Mlipo

Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
7,237
9,871
Kama magazeti ya Jitambue na Mshahuri Wako pamoja na Vitabu kv.Maisha na Mafanikio,nk ya marehemu Munga Tehnan vilibadirisha maisha yako ni wakati sasa wa kuungana pamoja.
Najua wengi mpo humu JF,ni rahisi sana kumtambua mwana utambuzi,naomba tuwasiliane. Asanteni.
 

mi mmojawapo.. Nilisikitika sana kusikia kifo cha yule jamaa.. Kwa kweli Taifa lilipoteza kichwa cha muhimu sana. Waliokuwa wakifuatilia mgazeti yale na vipindi vya luninga,wanaelewa ninachokisema...
 
mi mmojawapo.. Nilisikitika sana kusikia kifo cha yule jamaa.. Kwa kweli Taifa lilipoteza kichwa cha muhimu sana. Waliokuwa wakifuatilia mgazeti yale na vipindi vya luninga,wanaelewa ninachokisema...

Elimu ya Utambuzi idumu!Inatufundisha mambo mazuri!
 

Sikuwa mwanachama wa Jitambue. Ila nilikuwa msomaji mzuri sana wa magazeti ya Jitambue na Mshauri. Na haikuwahi kutokea nikakosa kusoma Jitambue. Hakika tumeikosa ladha tofauti na ya pekee. Vipi, kampuni ya TK MEDIA inataka kuanza uchapishaji upya? JITAMBUE, ni ladha tofauti na ya ukweli.
 

Dah!! Umenigusa paleple. Nimekuwa Mwanachama wa Miaka yoote. Lakini Kifo cha Munga kimetupokonya Mtu muhimu sana. Gazeti JITAMBUE lilitoa faraja kwa wenye Msiba, wenye shida na kila nyanja ya maisha. Lilitufanya tukubali hali halisi ya maisha tuliyonayo kwani lilitupa moyo. Niliwahi kumuuliza Mke wa Marehemu Munga kama kuna uwezekano wa kulirudisha mitaani akasema itachukua muda mreefu na ikishindikana litauzwa kwa mtu mwingine kuliendeleza. Hata hivyo alisema ataliuza kwa mwenye kuendeleza Elimu ya Utambuzi na sio Udaku.
 
 

Mimi pia sikuwa mwanachama bali msomaji tu wa kawaida. Najaribu kutumia JF kuwahimiza hata wale waliokuwa wakiandia makala kwenya magazeti hayo wajitokeze tuone la kufanya.
 
 
Elimu ya Utambuzi idumu!Inatufundisha mambo mazuri!

Nina maisha mazuri yenye malengo kwasababu ya JITAMBUE,ninautawala mwili wangu badala ya mwili kunitawala mimi....kila nikiangalia watanzania wenzangu kazini,majirani,abiria wenzangu ninapokuwa kwenye daladala na pia hapa JF nahisi japo kidogo nimeweza kuwa tofauti...Kwanini lakini tusiungane tukagawana hiki kidogo tulichojifunza?
 
Mimi pia sikuwa mwanachama bali msomaji tu wa kawaida. Najaribu kutumia JF kuwahimiza hata wale waliokuwa wakiandia makala kwenya magazeti hayo wajitokeze tuone la kufanya.

Bila shaka waliokuwa wakitoa Makala za Utambuzi wapo. Wajitokeze. Baadhi nawakumbuka kama Guru Francis. Shabani Kaluse, Haroun Janah, Stella Kamitu, Amri Gembe, Juma Yona na Asha Mkindi. Hawa woote walichangia kutoa Makala ktk Jitambue. Wako wapi? Kwanini wasikutane wakakubaliana kurudisha Gazeti la Jitambue hata kama ni kwa Sura nyingine? Watu tunalishwa Upuuzi kwenye Udaku.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…