Asante kwa andiko zuri, nimekisoma hiki kitabu cha Bishop Tutu pia.
Kuna sababu kwanini "Retributive justice" haijawahi kufanikiwa japo historia inatuambia mageuzi lazima yawe ya shuruti.
Protest and disruptions zinashurutisha na kulazimisha mageuzi (tunaweza kuchukua mfano wa South Africa na safari yao ya uhuru au recent example ya jirani zetu Kenya na safari yao ya machafuko na walivyopata katiba yao mpya).
Kama watanzania, ni muhimu kupaza sauti na kuwa clear kwamba tunachokipigania ni lazima kisikilizwe, ila baada ya hapo itahitajika strategy ya amani inayowezesha kusonga mbele na kua na mwanzo mpya.
Tukiendekeza visasi na kuamua kupambana wenyewe kwa wenyewe kwa damu na machozi basi tutapoteza na kuishia kuwa another Congo, au Somalia, au Sudan etc.